UTI inatokana na nini na kwanini inawa athiri zaidi wanawake

 UTI inatokana na nini na kwanini inawa athiri zaidi wanawake

UTI “maambukizi ya mfumo wa mkojo”, wengine huita “mchafuko wa mkojo” ni maambukizi ya sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo , sehemu za mfumo wa mkojo zinazoweza kuathiriwa na maambukizi haya ni figo, yureta, yurethra na kibofu cha mkojo. 

Maambukizi ya mrija wa mrija wa kutoleam mkojo “yurethra” huleta athari kama vile kuhisi kuungua wakati wa kukojoa,  kutoa mkojo mchafu “wenye rangi nyeupe” 

Maambukizi ya kibofu husababisha maumivu, nyuma ya mgongo, maumivu wakati wa kukojoa na damu kwenye mkojo, maumivu wakati wa kukojoa

Maambukizi kwenye figo huweza kusababisha maumivu ya mgongo, homa kali na kutapika

Kisababishi cha maambukizi ya mfumo wa mkojo

Kisababishi kikuu ni bacteria ambao maranyingi hutokana na uchafu unaotokea kwenye mfumo wa mmen’genyo wa chakula,wadudu hao hupitia mrija wa mkojo na kuweza kusambaa sehemu nyingine za mfumo wa mkojo

Kujamiiana pia ni nyia nyingine inayoweza kusambaa kwa maambukizi haya

Wanawake wanaathirika zaidi na maradhi haya kwa sababu ya “maumbile yao”  umbali mfupi kati ya mrija wa mkojo “urethra” na “sehemu ya haja kubwa”  hii husababisha uchafu kusafiri haraka toka kwenye sehemu hiyo na kuingia kwenye mfumo wa mkojo 

Ugonjwa huu hutibiwa kwa dawa za kuua bacteria “antibiotics”

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip