KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

 Tarakilishi/ kompyuta

Ni mashine ya kielektroniki yenye uwezo wa kipokea kichakata, kuhifadhi na kutoa taarifa kwa haraka kulingana na maelekezo

-Huwekwa programu  

-Hutumika kurahisisha kazi mbalimbali


Kazi za msingi za tarakilishi

Kuingiza au kupokea data au taarifa

Kutenda na kuchakata data au taarifa

Kuhudadhi data au taarifa

Kutoa au kuonesha matokeo ya kazi au taarifa


Aina za tarakilishi

Kuna aina mbili za tarakilishi: tarakilishi ya mezani na tarakilishi mpakato


Tarakilishi ya mezani

-Vifaaa vyake vimetenganishwa

-vifaa vyake ni kashamfumo, kibodi , kiteuzi na monita

Tarakilishi mpakato

-Vifaa vyake vyote vimeunganishwa

-Hurahisiha ubebaji na matumizi mahali popote


Kazi za vifaa vya tarakilishi

Kashamfumo :  Huifadhi na kulinda vifaa vyote vya kielektroniki

Kichakato kikuu :  hupokea na kuchakata kazi zote zinazoingia kwenye tarakilishi


Kiteuzi au mausi: Hutumia kielekezi kumwelekeza mtumiaji wa tarakilishi kuelekeza tendo fulani analotaka kufanya


Kibodi : Hutumika kuingiza data au taarifa kwenye tarakilishi. Data au taarifa zinazoingizwa ni tarakimu, herufi na alama maalumu za kiuandishi


Skrini au monita : Hutumika kuonesha kazi inayofanyika au taarifa iliyomo ndani ya tarakilishi


kitumi ingizi

- Kifaa kinachotumika kuingiza data au taarifa kwenye tarakilishi, mfano maikrofoni, kiteuzi, kinasa sauti na kibodi


Kitumi toleo

-kifaa kinachotoa taarifa toka kwenye tarakilishi mfano monita na ipaza sauti


Sehemu zinazounda tarakilishi

Tarakilishi imeundwa na sehemu kuu mbili, yaani maunzi na programu


Maunzi

-Inahusianisha sehemu sinazoshikika na zinazoonekana

-Mfano kiteuzi , monita, kipaza sauti, printa na kichakato kikuu


Programu

-hii inahusisha sehemu za tarakilishi zisizoshikika 

-ni mkusanyiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vya  tarakilishi vifanye kazi na kutoa matokeo kulingana na maelekezo

-Mfano ni programu endeshi na programu tumizi


Programu za tarakilishi

Programu ni seti ya maelekezo ambayo hutumika katika tarakilishi ili kufanya shughuri mbalimbali

-Aina mbili za programu zinazotumika katika tarakilishi ni hizi zifuatazo

Programu endeshi

-Programu hizi hudhibiti utendaji wa kazi zote ndani ya tarakilishi na hutawaka kazi zote zinazofanywa na vifaa vilivyounganishwa kwenye tarakilishi

Programu tumizi

Ni programu zinazomsaidia mtumiaji kufanya shughuli zake za kila siku, kw mfano kundika barua na ripoti, kusikiliza muziki, kuangalia picha za video na kuchakata hesabu.

-programu hizi jumuisha programu andishi na programu jendwali


Programu andishi

-Hutumika kwa ajili ya uchapaji wa nyaraka za aina mbalimbali kama vile barua, ripoti, makala na majarida

-huboresha waraka au wakala kwa namna mbalimbali 

-kubadili maandishi, kuongeza michoro, picha na majedwali yanayoendana na waeaka

-huonyehsa makosa ya kisarufi na tahajia unapokua unaandika


Sehemu za programu andishi

-hutegemea toleo lake

-Imejengwa na pau zana

-pau hizi zinamsaidia mtumiaji wa programu andishi kufanya kazi kwa urahisi

-pau zana zinazotumika mara kwa mara ni pau ya kawaida, pau ya mchoro, pau ya kuumbiza, pau ya sanaa matini, pau ya jedwali na kingo, pau ya fremu na pau ya barua pepe

-

Kazi mbali mbali kwenye programu andishi

Pau menyu

 - ina orodha ya majina ya menyu ambazo hutumika kuandaa nyaraka mbalimbali

- majina hayo ya menyu ni kama yafuatayo

 Faili, nyumbani, chomeka, sanifu, mpangilio wa ukurasa, marejeo, barua, pitia upya, mwonekano


-kila menyu huonesha utepe wenye mlolongo wa amri na picha au taswira zinazomwezesha mtumiaji kufanya kazi kwa urahisi zaide

-Pau menyu imeundwa na pau dogo zifuatazo

Faili:  menyu hii hutumika katika amri zote zinazohusu faili

   Menyu ya faili ina vipengele vifuatavyo

Nyuma: huoneshwa kea alama ya mshale ndani ya duara ambao mtumiaji hubofya endapo anahitaji kurudi nyuma katika dirisha la kuandikia

Taarifa: huonesha taarifa muhimu za faili au waraka kama vile jina, mwandishi, toleo la marekebishona tarehe ya marekebisho

Mapya: hutumika kufungua ukurasa wazi wa waraka

Hutumika kufunfua nyaraka zilizohifadhiwa ndani ya tarakilishi

Hifadhi : hutumika kuhidhi waraka kwa mara ya kwanza aukuhifadhi mabadiliko ya waraka unaofanyiwa kazi

Hifadhi kama. Hutumika kuhifadhi makala ya waraka au faili kwa jina lingine au sehemu nyingine ndani au nje ya tarakilishi

Chapisha: hutumika kuchapisha waraka katika printa au kuonesha mpangilio wa ukurasa utakavyoonekana baada ya kuchapisha

Shiriki: hutummika kushirikisha watu wengine kupokea, kuhariri au kutuma waraka

Hamisha : hutumika kubadili aina ya faili

Funga: hutumika kufunga faili au waraka uliofunguliwa

Nyumbani : huwezesha kuona ukurasa wa waraka na kufanya marekebisho katika mtindo au fonti tofauti katika aya auwaraka

Chomeka: hukupa fursa ya kuingiza vitu mbali mbali kama vile tarehe, namba za ukurasa au picha katika nyaraka

Sanifu : Hutoa fursa ya kurekebisha ukurasa kama vile kichwa cha habari aya, rangi na fonti

Mpangilio wa ukurasa : Husaidia kupanga mwonekano wa ukurasa 

Marejeo : hutumika kuborehsa kazi za uandishi wa taarifa kama vile yaliyomo, rejea na nukuu za vitabu

Barua : hutumika kuandaa na kupokea nakala nyingi za machapisho kwa wakati mmoja

Pitia upya : hutumika kusahihisha makosa katika waraka

Mwonekano : hukupa fursa ya kuona nyaraka katika sura mbali mbali

Zana za picha : hutumika kurekebisha picha katika mitindo tofauti

Pau ya kichwa cha habari

Huonesha jina la faili 

-Upandw wa kulia juu kuna picha za aikoni zinazotumika kushusha chini dirisha lililofunguliwa , kubadilisha ukubwa wa dirisha la kazi na kufunga dirisha la kazii

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip