FAHAMU MAGONJWA MAKUU YA NYANYA,DALILI NA TIBA ZAKE
FAHAMU.3. MAGONJWA MAKUU YA NYANYA,DALILI NA TIBA ZAKE
Magonjwa makuu ya nyanya ni kama yafuatayo:
1. Mnyauko Fusari (Fusarium wilt)
Kisababishi
Ugonjwa huu husababishwa na kuvu (Fungi) huenezwa na mbegu au udongo wenye vimelea vya ugonjwa. Ugonjwa hutokea zaidi wakati wa kiangazi na hasara inaweza kufikia hadi
asilimia 40 kama haukudhibitiwa.
Dalili zake
Mmea kunyauka ghafla wakati wa mchana na kurudia hali ya kawaida asubuhi. Baada ya siku chache mmea hufa. Shina la mmea likipasuliwa kwa urefu sehemu ya ndani huonyesha rangi ya kahawia.
Tiba yake
Ugonjwa huu hauna tiba maalum. Inashauriwa kutumia mbegu ambazo hazina ugonjwa, Panda nyanya kwa kutumia mzunguko wa mazao, dumisha usafi wa shamba kwa kuteketeza mabaki baada ya kuvuna, Mwagilia shamba mara kwa mara. Rutubisha vyema mimea na ondoa mar a moja mimea iliyoathirika.
2. Bakajani chelewa (Late Blight)
Kisababishi
Ugonjwa huu husababishwa na kuvu na huenezwa na upepo. Hasara inaweza kufikia asilimia mia moja kama unyevunyevu ni mwingi hewani.
Dalili zake
Madoa meusi kwenye majani, mashina na matunda, hatiamye majani yote hukauka na mmea hufa.
Nyanya zisizoiva huwa na mabaka magumu yenye rangi ya kahawia.
Nyanya zilizoiva huwa mabaka laini yenye rangi ya kahawia. Ukungu mweupe huonekana kuzunguka sehemu ya jani lililoungua.
Tiba yake
Fanya mzunguko wa mazao shambani na hakikisha kuwa nyanya au viazi mviringo havilimwi kwa kufuatana.
Punguza majani yaliyozeeka ili kudhibiti kiasi cha unyevunyevu shambani.
Nyunyizia dawa ya ukungu utakayoshauriwa
3. Bakajani tangulia (Early blight)
Dalili zake
Madoa meusi kwenye majani, mashina na matunda, hatimaye majani yote hukauka na mmea hufa. Nyanya zisizoiva huwa na mabaka magumu yenye rangi ya kahawia. Nyanya zilizoiva huwa mabaka laini yenye rangi ya kahawia. Ukungu mweupe huonekana kuzunguka sehemu ya
jani lililoungua.
Tiba yake
Fanya mzunguko wa mazao shambani na hakikisha kuwa nyanya au viazi mviringo havilimwi kwa kufuatana. Punguza majani yaliyozeeka ili kudhibiti kiasi cha unyevunyevu shambani. Nyunyizia dawa za ukungu utakazoshauriwa
4. Rasta (Tomato yellow leaf curl)
Kisababishi
Rasta husabishwa na vimelea vidogo sana na ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho wala darubini ya kawaida vijulikanavyo kama virusi. Shambani, hasa wakati wa kiangazi, ugonjwa huu husambazwa na wadudu aina ya nzi weupe. Rasta inaweza kusababisha hasara hadi asilimia 100 kama haikudhibitiwa mapema.
Dalili zake
Mmea hudumaa, na majani hupungua ukubwa, yanakuwa na rangi ya njano au zambarau na hujikunja kuelekea juu. Matunda huwa madogo sana, mengi hupasuka na huiva kabla ya kukomaa.
Tiba yake
Ugonjwa wa rasta hauna tiba. IIi kuzuia kuenea shambani inashauriwa kung'oa miche yote iliyoathirika na kuichoma moto. Pia kupulizia dawa ya kuua wadudu waenezao virusi vya ugonjwa huu na kuondoa magugu yote yanayozunguka shamba lako la nyanya. Hii husaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu.. Usivute sigara shambani. Epuka kushika mmea usiokua na ugonjwa baada ya kushika mmea ulioathirika na ugonjwa kwani kwa kufanya hivyo kunawezesha kusambaa kwa ugonjwa huo shambani. Puliza dawa ya kuua wadudu utakayoshauriwa
5. Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Kisababishi
Mnyauko bacteria husababishwa na bacteria na huenezwa na mbegu na udongo ulio na vimelea vya ugonjwa. Hasara inaweza kufikia hadi asilimia 40 kama ugonjwa haukudhibitiwa.
Dalili za ugonjwa
Mmea hulegea na majani hunyauka. Tofauti na mnyauko fusari ni kuwa shina likikatwa na utomvu wake ukikamuliwa kwenye chombo chenye maji meupe, maji hugeuka rangi na kuwa kama maziwa.
Tiba yake
• Panda mbegu zilizothibitish
• Tumia kiwango sahihi cha mbolea.
• Panda nyanya kutumia mzunguko wa mazao.
• Epuka kumwagilia maji yaliyopita kwenye shamba lililo na ugonjwa huu.
6. Batobato (Tomatomosaic virus)
Kisababishi
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na mbegu, kugusana kwa mimea au wakati wa kupogolea. Kiwango cha hasara kinaweza kufikia hadi asilimia 80.
Dalili za ugonjwa
• Mchanganyiko wa kijani kibichi na kijani kilichofifia hutokea kwenye majani.
• Kujikunjakunja kwa majani.
• Majani machanga huwa na maumbile yasiyo ya kawaida.
Tiba yake
• Tumia mbegu zilizothibitish
• Ng,oa mimea iliyougua mara tu ugonjwa unapotokea
• Teketeza mabaki ya mazao baada ya kuvuna
7. Ukungu mweupe (Powdery mildew)
Kisababishi
Ugonjwa huu husababishwa na kuvu na huenezwa na upepo, mvua pamoja na kugusana kwa mimea. Unaweza kusababisha hasara hadi asilimia 30.
Dalili za ugonjwa
Majani huwa na ungaunga mweupe kuanzia chini kwenye majani yaliyozeeka kwenda juu. Baadae majani hugeuka rangi na kuwa kahawia.
Tiba yake
• Tumia mbegu zenye kuhimili ugonjwa
• Puliza dawa ya ukungu utakayoshauriwa
Comments
Post a Comment