Huyu Ndo Rais Aliyekula Bata la Kutupwa Kuliko Marais Wote Duniani...Alijenga Paradiso Kijijini Kwake



ALIKUWA ni mmoja wa viongozi wa Afrika waliodaiwa kuwa wanapenda kuishi maisha ya anasa na kutumia vibaya fedha za nchi zao kwa kujinufaisha na mambo ambayo hayakuwa muhimu kwa watu wao ambao wanaendelea kuishi maisha ya umaskini.



Ni jamaa aliyekuwa anaitwa Joseph-Désiré Mobutu ambaye alikuja kubadili majina yake na kuwa Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Waza Banga. Alikuwa ni rais wa Zaire, nchi ambayo leo hii inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwaka 1965 hadi alipoangushwa mwaka 1997, akiwa mmoja wa marais waliotawala muda mrefu zaidi Afrika na duniani.


Mobutu aliyebadili jina la nchi hiyo kubwa na kuiita Zaire badala ya Congo mwaka 1971 na kuwataka raia wenzake kuachana na majina ya Kizungu na kuchukua ya Kiafrika mwaka huohuo, alikuwa ameamua kukipendelea kijiji cha nyumbani kwao kiitwacho Gbadolite (linatamkwa Gwadolite) na kukifanya paradiso ya Afrika na dunia.

Kijiji hicho kilichokuwa kidogo na ambacho kimezungukwa na misitu kiko pembeni kabisa, kaskazini mwa nchi hiyo kikipakana na Jamhuri ya

Afrika ya Kati, kilianzishiwa miradi mikubwa ya mabilioni ili kukipamba na kila aina ya anasa, yakiwemo mahoteli makubwa na uwanja mkubwa wa ndege ambao hata ‘madege’ makubwa aina ya Concorde yaliweza kutua.
Na ili kuhakikisha umeme ulikuwa unapatikana bila kipingamizi, Mobutu alijenga bwawa la umeme kwenye Mto Ubangi karibu na kijiji hicho na akajenga pia ikulu tatu tofauti kwa ajili yake na wageni wake kijijini hapo.

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip