Wanawake msichelewe kuzaa

Wanawake msichelewe kuzaa

Kuchelewa kuzaa kuna matatizo yake. Je unayafahamu?
Maelezo ya picha,

Kuchelewa kuzaa kuna matatizo yake. Je unayafahamu?


Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.

Athari za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Wanawake wengi wanaofanya kazi huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi wanapofika umri a miaka 35 badala ya kuzaa wakiwa na umri wa miaka 24-28.

Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya uzazi.

Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''

Bwana Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.

Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.

Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .

Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip