SABABU TISA KWA NINI WASOMI WENGI NI MASIKINI

SABABU TISA KWA NINI WASOMI WENGI NI MASKIN

Habari ndungu msomaji , leo tunaenda kuangalia kwa nini watu wengi pamoja na kwamba wamesoma sana lakini bado ni masikini sana. Tungetegemea kwamba baada ya mtu kupata digrii au PHD yake lazima afanikiwe sana kiuchumi lakini hali si hivyo. zifuatazo ni sababu tisa kwa nini wasomi wengi ni masikini
1. ELIMU YA FEDHA HAITOLEWI KWENYE TAASISI ZA ELIMU
Tunategemea kwamba shule lazima iwafundishe watu kila kitu kuhusu maisha lakini hilo si kweli, kwa mfano unaweza kuwa daktari mzuri lakini usiwe na uelewa wowote kuhusu pesa, waweza kuwa muhasibu unaehesabu pesa nyingi lakini bado usiwe na ufahamu wa kutosha kuhusu pesa. Sababu kuu ni kwamba shule hazikuanzishwa kwa ajili ya kuwafunza watu jkuhusu mafanikio au fedha. Suluhisho kwa hili ni kupata elimu ya kifedha kuhusu pesa kwa kusoma vitabu vizuri vinavyo  fundisha mambo ya kifedha. Unaweza kuvipaata baadhi ya vitabu hivyo kwenye website yetu
2. WASOMI WENGI HAWAJIENDELEZI KIELIMU BAADA YA KUPATA ELIMU YA MASHULENI NA VYUONI
Elimu kwa wengi ni digrii wanayopata baada ya chuo, wanadhani elimu ni vyeti vyao. Elimu sio kile unachopata darasani ,elimu ni kile unacho jifunza maishani , msomi wa kweli ni yule anayesoma kilasiku. Unatakiwa kuendelea kujifunza kila siku nyenzo za muhimu kwa ajili ya maisha. Wasomi wengi hawajifunzi mbinu mpya za kufanikiwaq kimaisha, mbinu mpya za kutafuta ela. suluhisho hapa ni kuon aelimu kama maji, jifunze kila siku
3.UNAPOZIDI KUPENZA KUKAA  SHULE NDIVYO UNAVYOZIDI KUPENDA KUAJILIWA
Shule zilitengenezwa ili kuwaandaa watu kuajiriwa. Ajira haiwezi kukufanya tajiri. Ajira inamaana utaendelea kufanya kazi na ubongo mmoja na mikono miwili, huwezi tengeneza utajiri kwa namna hii. Utajiri unatengenezwa ukiwa na watu wengi wanaokuzunguka.  unaweza kufanikiwa ukiwa mjasiria mali huku ukifanya kazi na watu wengi. Kila mmoja anaweza kuwa mjasiriamali kwa kujua umuhimu wa uwekezaji
4.WASOMI WENGI WANADHARAU
Wanaona kua wale ambao hawajasoma hawajui chochote na hivyo hawawezi kujifunza kwa watu hao, hata kama wamefanikiwa kiuchumi,  Mara nyingi waatu ambao hawajasoma ndio matajiri wanajua vitu avyingi ambavyo vyaweza kukusaidia.  Wasomi wengi wanaona haya kujifunza na kuendana na mabadiliko kwa kua wanaamini wao ni wasomi  kwa hio hawana haja ya kujifunza toka kwa wengine. Uwe tayari na ujifunze ili kupata mafanikio kiuchumi
5. WASSOMI WENGI WANANUNUA VITU VISIVYO INGIZA PESA
Vitu vingi wasomi wanavyonunua hawavihitaji, iphone, gari model mpya ni mfano wa vitu tunavyo vinunua lakini hjatuviitaji. Haijalishi unalipwa mshahara mkubwa kiasi gani kama una penda kununua vitu  visivyo vya muimu badala ya aset kama mashamba, huwezi kufanikiwa kiuchumi

6. WASOMI WENGI WANAFUKUZWA KAZI
Kwa uchumi wa sasa haijal;ishi ni elimu kiasi gani unacho, Chochote kinaweza kutokea na unaweza kufukuzwa kazi. Haimaanishi kua walio jiajiri hawafilisiki na kupoteza biashara zao hapana. mtu yoyote  anaweza kufilisika. Mjasiriamali amezoea mikiki mikiki  ya biashara na hata kama akipoteza biashara yake ana uwezo wa kuanza tena, kwa kua mjasiria mali anajua namna ya kuanza tena. Msomi hana jinsi baada ya kuopoteza kazi anafikilia kuanza kuomba kazi sehemu nyingine
7. MADENI YA VYUONI
Wanafunzi wengi wanasoma kwa msaada wa mikopo. Wasomi wanapo hitimu wengi wao wanaondoka wakiwa wanadaiwa pesa nyingi . Mfano mwanafunzi alie somea ualimu hupewa mkopo wa hadi milioni 13,  Wahitimu wa udaktari wanakdaiwa hata zaidi. Inachukua hadi miongo kadhaa kumaliza kulipa deni. Hili husababisha wengi kukwama kiuchumi
8.UNAVYOZIDI KUSOMA NDIVYO UNAVYOZIDI KUWA MPWEKE
Ili kutengeneza utajiri mkubwa lazima uwe na uwezo mkubwa wa kuungana na kufanya kazi na wengine, lazima ujue umuimu wa kushirikiana na watu, lazima uwe karibu na watu. Shule zinatufundisha kufanya kazi pekee bila kushirikisha watu, kufanya jaribio pekeeako na kufanya kazi pekeako. katika maisha unaitaji kuwa karibu na watu kuungana na watu unatakiwa kushirikiana na watu kutengeneza utajir
9. KODI IMETENGENEZWA KWA AJILI YA WASOMI
Kimsingi wasomi wenhi walioajiriwa wanatozwa kodi kubwa katika kipindi chao chooote wanachofanya kazi. Hii ni ani tofauti kwa wafanyabiashara na wajasiria mali ambao wanalipa kodi kidogo tu. Waajiriwa ndio wanotozwa kodi kubwa. Na ndio sababu kwa nini wengi wao ni masikini

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip