UJUE UGONJWA WA U.T.I (URINARY TRACT INFECTION)

  UJUE UGONJWA WA U.T.I (URINARY TRACT INFECTION)

U.T.I ni maambukizi kwa njia ya mkojo na huathiri mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi, wadudu huathiri sana kibofu na urethra. Jina U.T.I ni kifupi cha URINARY TRACT INFECTION (Neno la kingereza) watu wengi huzoea kuita hivyo wakijua ni jina la kiswahili, imeshazoeleka hivyo. Jinsia ya kike wana hatari kubwa kuliko jinsia ya kiume. Maambukizi yakwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea maambukizi yakifika mpaka kwenye figo. U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.

U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali, tunashauri mtu mwenye U.T.I inatakiwa awe msafi na kubadili mienendo iliyo hatarini.

UTI+Header

MGAWANYO WA U.T.I

Kuna mgawanyo wa aina mbili za U.T.I

  1. Maambukizi ya Upande wa juu – Hii hujumuisha Figo na Ureta
  2. Maambukizi ya Upande wa chini – Hii hujumuisha Kibofu na Urethra

CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA U.T.I

U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo, vitu vifuatavyo vinaweza kukuingiza kwenye hatari ya kupata U.T.I;

  1. Kinga ya mwili kuto kuwa imara
  2. Kutumia Vifaa au Dawa za kuzuia mimba
  3. Kwa wa kike; Kupungua kwa homoni ya estrogeni
  4. Mtu mwenye kisukari
  5. Kutumia choo kichafu na kutumia idadi kubwa ya watu
  6. Kuwa na tatizo la mmeng’enyo na tatizo la choo
  7. Kukaa kwa mda mrefu bila kutembeatembea

DALILI ZA MTU MWENYE U.T.I

Dalili za mtu mwenye tatizo la U.T.I hutokea tofauti kulingana na umri, jinsia na sehemu iliyoathiriwa. Hizo dalili ni kama;

urinary_tract_infections-1

  1. Kujihisi mchovu na kutokujisikia vizuri
  2. Kukojoa kwa shida na kujilazimisha
  3. Maumivu wakati wa kukojoa
  4. Kukojoa kiasi kidogo na mara kwa mara
  5. Mkojo kutoa harufu kali
  6. Mkojo kuwa na rangi tofauti zisizo za kawaida kwa mfano wekundu kiasi
  7. Kichefuchefu au kutapika
  8. Maumivu ya tumbo, au pande za mwili karibu na tumbo mpaka sehemu za misuli
  9. Joto laweza kuongezeka

JINSI YA KUEPUKANA NA U.T.I

  1. Kunywa maji mengi
  2. Acha kutumia dawa za uzazi wa mpango
  3. Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
  4. Kojoa hata kidogo baada ya kujamiiana
  5. Punguza au acha kunywa pombe na kutumia sigara huchochea kuathiri kibofu
  6. Kuwa msafi hasa sehemu za siri ili kutoruhusu bakteria
  7. Usipulizie spray kwenye sehemu za siri

TIBA YA UGONJWA WA U.T.I

U.T.I hutibika kwa kuwaondoa bakteria na fangasi sehemu zilizoathirika kwa kutumia dawa, mtu mwenye U.T.I hupata shida sana na mpaka humpelekea kutokuwa na raha. Mtu mwenye U.T.I asipoitibu husababisha vimelea kuzaliana na kuwa vingi hii huitwa U.T.I sugu yuko hatarini kuwa na tatizo kubwa na pia hukaribisha magonjwa mengi

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children