UKWELI KIHUSU SAMAKI NGUVA

UKWELI KIHUSU SAMAKI NGUVA .(Samaki mtu).



Watu wengi hawajui uhalisi wa mnyama huo kwani
baadhi ya watu wamekuwa wakisema ni upande
mmoja samaki na mwingine mwanamke.

Makumbusho ya taifa ambayo ndiyo ina dhamana
ya kuhifadhi mambo ya kale imeweka wazi ukweli
kuhusu nguva na maisha yake . Mkurugenzi wa
Makumbusho hayo , Bw . Paul Msemwa , anasema
mnyama huyo mambo mengi ambayo yamekuwa
yakizungumzwa kuhusu mnyama huyo si ya kweli .
Anasema nguva ni mnyama anayezaa na
kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine.

Anasema wakati akinyonyesha husimama na
kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya
mtu aliyemuona kudhani kuwa ni mtu.

Anaeleza kuwa watu wengi hawajui ukweli kuhusu
nguva na baadhi wamekuwa wakisema kuwa ni
nusu mtu. `` Kuna watu wanapotosha wanasema
nguva ni nusu mtu kwa maana kuwa chini ni
samaki na juu ni mtu lakini si kweli ,`` anasema .

Anasema muda mrefu mnyama huyo hukaa
baharini na kwamba anapenda mazingira mazuri na
tulivu. Dk . Msemwa anasema mnyama huyo huzaa
kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto
mmoja pekee . Mtoto wa mnyama huyo
anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153 hadi 200 ,
wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400
hadi 1 , 000 . Dk. Msemwa anataja maeneo ambayo
wanyama hao hupatikana kuwa ni Somanga karibu
na Rufiji , Kilwa , Mafia , Moa Mombasa, Tanga na
Bagamoyo.

Anasema endapo mazingira ya bahari yataendelea
kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho
kutoweka. Alisema kwa kawaida nguva hupenda
maeneo tulivu na yasiyo na vitisho .

``Huu uvuvi haramu wa mabomu na baruti
utasababisha wanyama hawa kutoweka kabisa
kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa, ``
anasema. Anasema mnyama huyo hupendelea
zaidi kula majani yaliyo chini ya bahari maarufu
kama mwani.

Nguva ana rangi ya kijivu na umbo la mwili wake
ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe.

Awapo katika maji hutoa kichwa chake juu ya maji
kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua
yaliyopo upande wa juu wa kichwa chake. Dk .
Msemwa anasema nguva jike ana chuchu kifuani
na anaponyonyesha mwanaye husimama kwa
kutumia mkia wake chini na kumkumbatia
mwanaye kama binadamu. Aidha , anasema tayari
wameanza kuwaelimisha wavuvi kuhusu mnyama
huyo ili wamwonapo wasimvue.

Anasema kuna wakati wavuvi walikuwa
wakiwavua na kuwala kwa kuwa nyama yao ni
tamu zaidi ya ile ya ng? ombe . Anasema kutokana
na mazingira kuharibiwa, hivi sasa mnyama huyo
ameanza kutoweka sehemu ambazo alikuwa
akionekana.

``Alikuwa akionekana Dar es Salaam , Kimbiji,
Buyuni, lakini sasa haonekani tena na hali hii
inatokana na usumbufu wa wavuvi na mazingira ya
bahari kuchafuliwa, `` anasema .

Anasema mnyama huyo ana aibu na anapogundua
kuwa maeneo alipo kuna binadamu huhama na
kwenda mbali zaidi . Dk . Msemwa anasema vifo
vya nguva vimekuwa vikitokana na ajali za bahati
mbaya mfano kunaswa kwenye vyombo vya
kuvulia kama vile jarife , mishipi na kuongezeka
kwa shughuli za uvuvi .

Kwa upande wake , Mkuu wa Idara ya Viumbe
katika makumbusho hayo , Bi. Adelaide Sailema
alisema wameanza kuelimisha wavuvi ili
wanapowaona wanyama hao wasiwavue .
Anasema kuna umuhimu wa kuweka maeneo
tengefu kwa ajili ya kuwahifadhi wanyama hao .
``Tumeishauri serikali itenge maeneo ambayo
mnyama huyo anapatikana ili wasitoweke ,``
anasema. Anafafanua kuwa mtawanyiko wa nguva
upo zaidi maeneo ya Somanga , Kilwa , delta ya
Rufiji, Mohoro na Mafia kuanzia miaka ya 1960 .

Anasema nguva amekuwa akionekana mara nyingi
zaidi miaka ya 1950 sehemu za Kilwa Kivinje miaka
ya 1960 sehemu za Mkwaja na Matapata miaka ya
1970 sehemu za Kilwa kisiwani, Kilwa Masoko na
kaole miaka ya 1980 sehemu za Somanga ,
Pombwe na Olelo miaka ya 1990 sehemu za
Masoko Pwani na miaka ya 2000 sehemu za
Somanga , Utigi Ngolwe , Pombwe na Mbonde.
Sehemu zingine zilizoripotiwa kuwa na nguva ni
Lamu , pangani, Tanga, Buyuni, Kimbiji, Unguja ,
Pemba, Mafia na Kisiju . Dk . Msemwa anasema
nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa
manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho .

Wakati huo huo , anasema ukumbi wa kudumu wa viumbe
(biolojia ) ni kati ya kumbi nne za kudumu zilizopo
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni .

Anasema ukumbi huo ulianzishwa rasmi mwaka
1980 baada ya kumbi nyingine kuwepo ambazo ni
ukumbi wa chimbuko la Mwanadamu , ukumbi wa
historia ya Tanzania na ukumbi wa mila na desturi
za Mtanzania . Anasema ukumbi wa viumbe
ulipoanzishwa ulilenga zaidi maonyesho ya viumbe
bahari na mara nyingi ulijulikana ukumbi wa
viumbe bahari ( Marine Biology Gallery ).
Anasema moja ya maonyesho yaliyopo katika
ukumbi huo ni maonyesho ya mnyama Nguva
ambaye kwa mara nyingi amekuwa akiamisha
maswali na majibu ya aina mbalimbali kutoka
katika jamii kama ni nusu samaki na nusu
mwanamke.

Anaeleza kuwa kutokana na mahitaji mbalimbali ya
jamii yaliyojitokeza , ilionekana kuwa ni sahihi kuwa
na viumbe kutoka katika mifumo ikolojia
mbalimbali ili kuweza kukidhi haja. Anasema kwa
sasa mikusanyo iliyopo imegawanyika katika
sehemu kuu tatu kutokana na mifumo ikolojia
ilikotoka mikusanyo hiyo .
Anatoa mfano wa mfumo ikolojia wa bahari Wenye
wanyama wanyonyeshao , samaki, kamba kochi ,
kasapweza, miamba ya matumbawe , majongoo
bahari, konokono na kaa .

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children