UKIONA DALILI HIZI ZA MWANZO KAPIME UKIMWI FASTAAA: ZAWEZA JIONYESHA BAADA YA WIKI MBILI


Watu wengi wamekuwa waoga kupima virusi vya Ukimwi kutokana na madhara ya kisaikolojia yanayojitokeza baada ya mtu kujijua ana ugonjwa huu, hivyo wengi huamua kubaki na sintofahamu tu. Kwa ambao hawajawa tayari kupima Ukimwi, dalili zifuatazo zinaweza kuwa za ugonjwa wa Ukimwi
Watu wengi wamekuwa waoga kupima virusi vya Ukimwi kutokana na madhara ya kisaikolojia yanayojitokeza baada ya mtu kujijua ana ugonjwa huu, hivyo wengi huamua kubaki na sintofahamu tu. Kwa ambao hawajawa tayari kupima Ukimwi, dalili zifuatazo zinaweza kuwa za ugonjwa wa Ukimwi.
Maumivu ya koo na kichwa yanayodumu. Ni kawaida sana kupata maumivu ya kichwa na koo yanayodumu ambayo mara nyingi yanasababishwa na magonjwa ya muda mfupi kama malaria na mengineyo, maumivu ya koo na kichwa mara tu baada ya kupona magonjwa hayo ya muda mfupi.
Pia maumivu ya koo na kichwa yanayodumu muda mrefu yanaweza kuwa ishara ya maambukizi ya Ukimwi, mathalani yakidumu muda mrefu kwa mtu ambaye hajapima virusi vya Ukimwi na hajajua kama ameshaambukizwa au la. Mbaya zaidi ikitokea mtu anayepata dalili hizi awe amewahi kufanya ngono bila kinga na idadi kadhaa ya watu kwa miezi ya karibuni.
Afya ya ngozi kubadilika. Miezi michache baada maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kuna baadhi ya ishara zinaweza kujionyesha kwenye ngozi.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, virusi vya Ukimwi vinaenda kupambana na mfumo wa kinga mwilini, mfumo huo ukizidiwa nguvu na virusi ndipo Ukimwi unapoanza kuathiri afya ya mwili mzima ikiwemo afya ya ngozi.

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children