Chaja isiyotumia waya “wireless charger” inafanyaje kazi

  Chaja isiyotumia waya “wireless charger” inafanyaje kazi




Bila shaka umekwisha sikia kuhusiana na mfumo mpya wa kuchaji vifaa vya umeme (kama simu, saa, radio, n.k) bila kutumia waya uliounganishwa moja kwa moja

Hii ni teknolojia mpya inayokua kwa kasi zaidi katika siku za hivi karibuni hasa inatekelezwa na makampuni ya kutengeneza simu kama vile “apple” kwenye sim zake za Iphone x na Iphone 8, kampuni inayotengeneza simu zenye mfumo wa android ya Samsung pia imetumia mfumo huu kwenye simu zake za galaxy note 8  galaxy s8 na galaxy s7

Kuchaji bila chaja “wireless charging” ni mfumo wa kuchaji vifaa (kwa mfano simu) unao kuwezesha kuchaji kifaa chako bila kuunga waya moja kwa moja kutoka kwenye plagi ya ukutani

Kimsingi bado waya unatumika isipokua, kunakua hakuna muunganiko wa moja kwa moja kati ya simu yako na chaja.

Chaja zisizotumia waya “wireless chargers” zimatumia mbinu inayoitwa kwa kimombo “magnetic induction” yaani “kuingizwa usumaku” , pia kuna mbinu inayo itwa “magnetic reasonance” ambayo nayo inatumiwa na chaja hizi. Leo tutaangazia zaidi teknolojia ya “magnetic Induction”

“magnetic induction” ni uzalishaji wa umeme au hali ya usumaku bila kugusanisha kifaa  cha umeme au kifaa chenye usumaku

Kimsingi kwa kutumia njia hii ya “magnetic induction” una uwezo wa kuzalisha umeme toka kwenye sumaku bila kuvi gusanisha vitu hivyo pamoja

Chaja inafanyaje kazi ?

Kimsingi inatumia waya pia

Chaja  isiyo tumia waya “wireless charger” lazima ichomekwe kwenye plagi ya umeme ukutani, waya kutoka kwenye plagi ya umeme umeungana na kifaa bapa kinachoitwa “charger pad” ambacho juu yake ndipo unapo ilaza simu yako ili iweze kuchajiwa.

Chaja hizi hutumia kuingizwa kwa usumaku “magnetic induction” kama nilivyo eleza hapo awali 

Chaja hizi zinatumia usumaku  toka kwenye bapa la kuchajia “charger pad” na usumaku huo hubadilishwa kuwa umeme unaotumika kuchajia simu

Kwanza unaweka simu juu  bapa la kuchajia “charger pad” 

Mkondo wa umeme “current” unasafiri kupitia kwenye waya , toka kwenye plagi ya ukutani  hadi kwenye bapa la kuchajia, 

Ndani ya bapa la kuchajia “charger pad” kuna vifaa ambavyo hubadili mkondo huo wa umeme na kutengeneza eneo la nguvu ya usumaku “magnetic field” au usumaku

Ndani ya simu (yenye uwezo wa kuchajiwa na chaja hii) kuna kifaa cha kubadili usumaku toka kwenye bapa la kuchajia kuwa mkondo wa umeme

Eneo la usumaku “electric field” toka kwenye bapa la chaja hubadilishwa kwa kutumia koili iliyo ndani ya simu  kutengeneza mkondo wa umeme. Simu lazima ilazwe juu ya bapa la kuchajia “charging pad” na lazima iwe karibu zaidi kwani ufanisi wa chaja hii unapungua simu inapo kua mbali

Kwahio nishati ya usumaku kwenye chaja inabadilishwa kuwa nishati ya umeme kwenye simu ambayo ndiyo inayotumika kuchajia betri la simu


Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children