Kansa ya shingo ya kizazi “cervical cancer”

 Kansa ya shingo ya kizazi “cervical cancer”



Hii ni kansa ya seviksi (au shingo ya kizazi)

Seviksi ni sehemy ya chini ya tumbo la uzazi  inayo ungana na mlango wa uzazi (uke)

Ni kansa inayo athiri wanawake wengi zaidi duniani kuliko kansa zingine za uzazi

Lakini kansa hii inaweza kuzuiwa kama itagundulika mapema na pia kuna chanjo ya kuua vijidudu vinavyosababisha kansa hii

Seviksi imeundwa na seli za aina mbili : seli za tabaka la juu “squamous cell” na seli za tabaka la chini “grandular cell” 

Seli zote hizi zinaweza kuathiriwa na kansa, seli za tabaka la juu “grandular cell” ndizo huathiriwa zaidi

Kansa mara nyingi huanza eneo la shingo ya kizazi ambapo aina mbili za seli hizi hukutana “transformation zone”

Kirusi aina ya HPV (human papilloma virus) ndicho kisababishi kikuu cha kansa ya kizazi

Kuna zaidi ya aina mia moja ya virusi hivi. Lakini asilimia sabini ya kansa ya seviksi husababishwa na aina mbili za virusi vya HPV , aina hizo ni HPV 16  na HPV 18

Protini mbili zinazozalishwa na virushi vya HPV (majina ya protini hizo kwa kifupi “E na E7”) ndizo zinazo sababisha tatizo la kansa kutokea

Protini hizo huzuia jeni “gene” inayotumiwa na seli za shingo ya kizazi “kuzuia seli hizo kujigawa bila mpangilio”

Hii husababisha seli kujigawa bila mpangilio na kusababisha uvimbe wa kansa

Virusi vya HPV huambukizwa kwa njia ya kujamiiana

Kwa wanawake wengi virusi vya HPV hukabiliwa na mfumo wa kinga wa mwili na kuzuia kupata kansa

Mambo yanayoweza kuchangia kushambuliwa na virusi hivi vya HPV na kupata kansa ni kama vile kuwa na kinga dhaifu (kutokana na maradhi kama vile VVU) magonjwa ya ngono, uvutaji sigara, kuzaa watoto wengi na pia matumizi ya mda mrefu ya vidonge vya uzazi

Dalili za kansa 

Hatua za mwanzo za kansa hii huwa hazionyeshi dalili

Kansa hii inapokua na kuanza kuenea dalili hizi hutokea, kutokwa na damu (baada ya kujamiiana, kabla  na baada ya hedhi), maumivu makali ya tumbo (wakati wa tendo la ndoa) kutokwa na maji eneo la uke

Ili kuweza kuchunguza ikiwa umeathiriwa na virusi hivi vya HPV au una hatari ya kupata kansa ya shingo ya kizazi, daktari atachukua kipimo kinachoitwa “pap test” hiki ni kipimo kinacho husisha kuchukua baadhi ya seli za shingo ya kizazi ili kuzichunguza kama zimeathirika na kansa

Kipimo cha “HPV DNA test” ni kipimo cha damu kinachotumika kubaini uwepo wa vinasaba “dna” vya kirusi cha HPV , kipimo hiki hutumika kubaini kama umeambukizwa virusi vya HPV

Matibabu ya kansa hii huusisha  njia kama vile : upasuaji( ili kuondoa seviksi na tumbo la uzazi) , matumizi ya mionzi kuua seli za kansa yaani “radiation” na matumizi ya kemikali kuua seli za kansa yaani “chemotherapy”


Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip