Vitunza taarifa kwenye kompyuta “storage devices”
Vitunza taarifa kwenye kompyuta “storage devices”
Kompyuta ina aina mbili za memori
(a) “primary memory
Hii ni memori inayotunza taarifa kwa muda mfupi ,
Unapozima kompyuta yako taarifa zilizo tunzwa kwenye memori hii “ram” hufutika moja kwa moja
Kwa mfano kama ulifungua programu ya “Microsoft office “ ukawa unaandika kitu , taarifa ya program hio inakua imetunzwa kwenye ramu, kama kompyuta yako itazima ghafla ina maana kila kitu ulicho andika kitafutika
Lakini kama ume tunza yaani ume “save” ina maana taarifa itaenda kwenye memori ya kutunzia documenti yaani “secondary storage”
ramu, inatunza taarifa za kompyuta pale tu unapokua umewasha kompyuta yako
(b) Seconday memory
Hii ni memori ya moja kwa moja
Hapa tunazungumzia “hard disk”
Kila kompyuta inaitaji sehemu ya kutunza taarifa kama vile picha , document na mfumo endeshi wa kompyuta, kompyuta inahitaji sehemu ya kutunza taarifa hizi kwenye “storage drive”
Memori hizi hazifuti taarifa, zitaendelea kutunza taarifa hata kama utazima kompyuta
Kuna aina tofauti za memori hizi “internal storage drives”
Zinaweza kua "magnetic storage drive" , "solid state drive"
(a) Magnetic hard drive
Hii ni memori ya ndani ya kompyuta iliyo undwa na disk zenye sumaku, ina
Hii imegunduliwa mwaka 195
Imefunikwa kwenye kiboksi kilichofungwa “sealed case” ,ndani yake ina disk zenye usumaku
Kwenye hizi disk ndipo ambapo taarifa “data” zinapotunzwa
Disk hizi huzunguka kwa spidi kubwa , na zinapozunguka ndipo ambapo mchakato wa kusoma taarifa “reading of data” na kutunzwa kwa taarifa yaani “writing of data” unapofanyika kwenye disk
Disk hutumia kebo “SATA cable” ambayo hutumika kusafirisha taarifa kati ya hard disk na sehemu zingine za kompyta
(b)Solid state drive “haina sehemu inayo zunguka “
Hizi memori “drives” hazina sehemu zinazo zunguka
Hizi memori “drives” zinatumia chip ndogondogo za memori / vimemori vidogodogo, kama vile unavoviona kwenye flashi “flash momory chips” kutunza taarifa za kompyuta
Taarifa huweza kusafirishwa haraka sana
Kwa kua hazina sehemu zinazo zunguka , hazitoi sauti, na pia hazitumii umeme mwingi kwa sababu hio
SSD haziwezi kuharibika haraka kwa sababu ya mitikisiko au kuanguka kwa kua hazina sehemu zinazo zunguka zaidi ya
SSD ni ghali zaidi
SSD zina ufanisi na spidi kubwa zaidi , ukitumia SSD inamaana spidi ya kompyuta yako itaongezeka
Matumizi ya SSD huongeza ufanisi na spidi kwenye kompyuta, unaweza kuongeza ramu , mpaka GB8 lakini kama “hard disk “ yako inakua ina spid ndogo usitegemee mabadiliko makubwa
Comments
Post a Comment