Fahamu kuhusu ugonjwa wa fangasi aina ya kandidiasisi

 Fahamu kuhusu ugonjwa wa fangasi aina ya  kandidiasisi

Kandidiasisi ni maambukizi ya fangasia au kuvu yanayotokana na aina yoyote ya kandida (aina ya chachu)

Maambkizi hayo yanapoathiri kinywa kwa kawaida huitwa kandidiasisi ya kinywa. Ishara na dalili zinajumuihhsa madoa meupe kwenye ulimi au sehemu nyingine za kinywa na koo. Dalili nyingine zinaweza kujumuisha maumivu na matatizo wakati wa kumeza

Maambukizi hayo yanapoathiri uke kwa kawaida huitwa maambukizi ya chachu. Ishara na dalili zinajumuisha kujikuna kwenye uke, mwasho na wakati mwingine mchozo mweupe unaofanana na jibini kutoka ukeni. Kwa nadra uume unaweza kuathirika na kusababisha kujikuna.

Kwa nadra sana maambukizi hayo yanaweza vamia na kuendea kwenye mwili wote na kusababisha homa pamoja na dalili kulingana na sehemu za mwili zilizoathiriwa

Kisababishi

Kuna aina 20 za kandida zinazoweza kusababisha maambukizi huku “candida albicans” ikitokea mara nyingi zaidi. Maambukizi ya kinywa hutokea mara nyingi kwa watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja, wazee na walio na mfumo dhaifu wa kingamaradhi. Hali zinazosababisha mifumo dhaifu ya mwili zinajumuisha UKIMWI , upandikizaji wa ogani, kisukari na matutmizi ya kotikosteroidi, Hatari nyingine zinajumuisha meno bandia na kutumia antibiotiki

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children