Jinsi ya kuongeza thamani yako by joel nanauka

 Jinsi ya kuongeza thamani yako by joel nanauka

Tutajikita kujifunza namna ya kuongeza thamani katika kile tunachokifanya na zaidi kuongeza thamani kwetu sisi wenyewe. Wewe kama mwanadamu thamani yako inaweza kuongezeka kama una uza bidhaa au una huduma ama una kipaji , unaweza kuongeza thamani yako katika kile unachokifanya na kufanikiwa zaidi

Je unafikili thamani ya mtu ina bebwa na nini?

Kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye somo la jinsi ya kuongeza thamani ni vema uka lijua hili

Ningependa kuanza na nukuu “quotation” ninayopenda sana kuitumia inapofika kwenye swala la kuongeza thamani “kwenye ulimwengu wa sasa haulipwi kwa muda unaoutumia bali unalipwa kwa thamani ambayo unaitoa”

Hii ni muhimu sana kwa sababu kuna watu wanafikili kwamba ili kufanikiwa zaidi wanaitaji kuongeza muda wa kufanya kazi, kufanya kazi kwa muda mrefu ni muhimu lakini  hilo pekeake halitoshi kukufanya wewe ulipwe zaidi , kwa mfano kuna watu wanafanya kazi mda mrefu sana kama walinzi wanafanya kazi mda mrefu lakini wanalipwa kidogo sana

Leo utajifunza vitu vitatu vikubwa

1.  Utajifunza maeneo mkakati makuu kwa ajili ya thamani yako “key strategic area to increase your values”

2. 2.  Vitu vinavyo shikilia thamani yako

3. Unawezaje kuongeza thamani yako 

Tuangalie vitu vinavyo shikilia thamani yako 

Hapa ni vema kujikagua kuona ni vitu gani vinashikilia thamani yako

(a) Ujuzi “skill or competence”

Ujuzi ni uwezo wako wa kufanya kitu, hii ni zaidi ya kujua “Yaani kufahamu kuhusiana na kitu Fulani”

Kwenye ujuzi unaweza kuongeza thamani yako hapa kuna vitu unatakiwa kufanya ili kuongeza ujuzi wako 

Cha kwanza ni kwamba katika kila kitu unachofanya kuna kitu kinaitwa “competence framework”  maanya yake ni aina ya ujuzi unaotakiwa kuwa nao katika kile kitu unachokifanya ili ukifanye kwa thamani kubwa sana 

Katika kitu unacho kifanya kuna aina za ujuzi kama tatu, nne tano mpaka saba za ujuzi unazotakiwa kuwa nao kwa hio ni muhimu sana.

Kuna watu ambao thamani zao zimeshikiliwa katika ujuzi walio nao pengine ni ujuzi wa kucheza mpira pengine ni ujuzi wa kutengeneza gari 

Ujuzi unaweza kujifunza kwa njia ya kusomea au “experience”

Eneo la pili ni mtandao wako “professional network” kuna watu ambao thamani yao imebebwa kwenye mtandao walio nao , 

Mtandao wako ni aina ya watu wanaokuzunguka, watu unaofaamiana nao,  watu wanao kuheshimu na wewe unao waheshimu, 

Mtandao umegawanyika katika sehemu kuu mbili

“vertical network “ ni mtandao wa watu walio juu zaidi yako , kuna watu ambao thamani na mafanikio yao yamebebwa na watu ambao wako juu zaidi yao ki uchumi na ki madaraka. Watu hao uki wahitaji unaweza kuwafahamu

“horizontal network” ni mtandao wa watu ambao wako “level” sawa na wewe, kwa mfano wewe ni mfanya biashara na una mtandao mkubwa wa wafanyabiashara wenzako , unaweza hata pata bidhaa bila tatizo kwa sababu unafahamiana na wafanyabiashara wengi zaidi

Eneo la tatu “strategic area” ya kutengeneza thamani yako ni kutumia “brand yako” hii ni thamani yako katika jamii, jinsi ambavyo unajulikana au kufahamika na watu, vile unavyo onekana

 Muanzilishi wa amazon aliwahi kusema kua “brand” yako  ni kile kitu ambacho watu wanasema kuhusu wewe unapokua haupo, vitu vinavyo jenga “brand” yako ni hivi vitatu

Cha kwanza “image” yaani muonekano wako, unavyo tokea mbele za watu , watu wana kuonaje , tafiti zina sema kwamba zile dakika chache za mwanzo unapokutana na watu mara nyingi wana fanya “conclution” juu yako , kuanzia ulivyo vaa, muonekano wako, unavyotembea

Ndio maana tunasema lazima uvae kwa namna unavyotaka watu wa “ku address” kwenye maisha yako

Cha pili “repeatataion” watu wana sema nini kuhusu wewe, ni kitu gani ambacho watu wana zungumza kuhusiana na wewe . Fursa tunazo zitafuta zipo mikononi mwa watu kwa hio kile watu wanacho kisema tunapokua hatupo nao kina maana kubwa sana, kina julisha kama uta  endelea kupata fursa au hautaendelea kupata fursa

Cha tatu ni “character” ni vile ambavyou upo, vile ambavyo unajulikana uhalisia wako ni kama tunavyosema “a, b, c, d” hauwezi badili character yako neneo hili lina asili ya kigiriki inayo maanisha “statue” yaani sanamu. Huu ni uhalisia wako hauwezi badilika kirahisi

Tuangalie maeneo yanayoshikilia thamani yako 

Ni muhimu kujua kitu gani kinachoshikilia thamani yako

Vitu vitatu vikubwa vinavyo shikilia thamani yako ni hivi vifuatavyo

1. Upekee wako

2. Ni ngumu kiasi gani kupata mbadala wako, inavyokua ngumu kupata mbadala wa wewe thamani yako inaongezeka, kadili inavyokua ngumu kupata bidhaa unazouza ndio thamani yako inavyo ongezeka zaidi, ni nini hasa kinakutofautisha

Hii ndio sababu kwa nini dhahabu ina thamani kubwa, ni kwa sababu ni ngumu sana kuipata

Upekee wako  inawe  kuwa kwenye “utoaji bora wa huduma” ama kwenye “uharaka wa huduma zako” ama kwenye sehemu yoyote ile. Lazima ujue kua upekee wako upo wapi, inakua ngumu kupata mbadala wako , 

3. Ubora wa kile unachofanya 

Oprah winfrey alisema “Nilikuzwa nikiambiwa kuwa nikiwa bora katika ninachofanya hakuna atakae nibagua kwa sababu ya rangi yangu ama jinsia yangu”

Ubora unafanya udhaifu wako ufunikwe, ubora unashikilia thamani yako, utakataliwa kama hujafikia ubora unaotakiwa.

Ubora unashikilia thamani yako

4. Consistency “kufanya kwa muendelezo”

Ni jinsi ambavyo unaweza ukaaminika, 

Maranyingi watu wengi wanafanya vitu na kuishia njiani, 

Kama wewe ni mtu unae anza na kushindwa kumaliza huwezi kuwa bora katika kile unachofanya

Kuna vitu ambavyo matokeo yake hutayaona karibuni, kwa hio ni vizuri uka fanya kwa muendelezo, 

Kufanya kwa muendelezo ni ngumu sana pale unapofanya na hakuna mtu anaekuangalia , lakini unatakiwa ufanye vitu kwa muendelezo bila kusita ama kuacha kwa sababu unapofanya vitu kwa muendelezo unafanya kwa ajili yako wewe mwenyewe, unafanya kwa faida yako wewe mwenyewe

Tunavutiwa na “decipline” za watu

Chochote unachofanya jitahidi kufanya kwa muendelezo bila kukata tama


Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip