Siri moja ambayo wajasiriamali pekee wanaijua kuhusu pesa

 


Siri moja ambayo wajasiriamali pekee wanafahamu kuhusu pesa

Wiki chache zilizopita nilikua na kikao na mfanyabiashara mmoja aliekua akijaribu kunishirikisha ‘mpango wa kibiashara’ nami, baada ya kusikiliza mipango yake niligundua kitu ambacho “si cha kijasiriamali” kwenye mpango wake ambacho kilikua ni “kufanya kazi kwa ajili ya kila shilingi anayo itengeneza” hivi si ambavyo wajasiria mali wa kweli wanavyotengeneza biashara na pesa zao

Wafanya kazi wanafanya kazi kwa kila shilingi wanayoitengeneza , wajasiriamali wanatengeneza mifumo inayo wachapishia pesa zaidi ya wanayoifanyia kazi

Nita shiriki nawe siri moja ambayo wajasiriamali wanaifahamu kuhusu pesa

Fikiria hili madaktari, mainjinia, na wahasibu wanatengeneza pesa nyingi kwa mwezi, lakini lazima wafanyekazi kwa kila shilingi wanayo itengeneza, wanafanya kazi kwa ajili ya kipato cha mwezi kwa hio wanapata pesa kutokana na kuweka masaa mengi kwenye kazi wanazofanya. Hii ndiyo sababu waajiriwa wengi si mitajiri

Fikiria kuhusu wajasiriamali ,mjasiriamali wa kweli anafanya kazi kwa bidii kama mtu yeyote lakini hafanyi kazi kwa ajili ya mshahara “kipato cha mwezi” ana tengeneza mali “assets” 

Tofauti hapa ni kwamba unapofanya kazi kwa ajili ya “ujira” au “kipato cha mwezi” unapata pesa kwa kukamilisha “majukumu Fulani” ndani ya muda Fulani kama vile wiki au mwezi  lakini uki fanya kazi kwa ajili ya “asset” inamaana unaweza kufanya kazi kwa bidii kwa miezi au miaka kadhaa bila ya “mshahara”  lakini hizi “asset” unazozitengeneza zikisha simama imara zinaweza kuendelea kukuzalishia pesa kwa miaka mingine mingi zaidi ijayo

Baadhi ya bidhaa “product” zangu nilizitengeneza miaka mitatu iliyopita lakini zinaendelea kunizalishia pesa mpaka sasa, kunaweza kua na marekebisho ya hapa na pale lakini bado nina uwezo wa kuendelea kutengeneza pesa.

Karibu kila mmoja anafanya kazi kwa ajili ya “kipato” mjasiriamali  anafanya kazi kutengeneza “asset” na ndio sababu wengi wao ni matajiri

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children