Kiharusi ni ugonjwa wa aina gani

 




Kiharusi ni ugonjwa wa aina gani

Kiharusi (kwa kiingereza stroke) ni ugonjwa unaoleta hali ya mwili kupooza kutokana na matatizo kwenye mishipa ya damu inayolisha ubongo.

Katika tiba kiharusi ni upotevu wa uwezo wa ubongo unaoendelea haraka.

Sababu ya ugonjwa huo ni tatizo katika mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo.

Matatizo hayo ni ama kuzibwa ama kupasuka kwa mishipa ya damu.

Seli za ubongo hufa haraka zisipopata oksijeni na lishe ya kawaida ambayo yote haya hufika kwa njia ya damu. Kiharusi ni hali ya dharura inayoweza kutibiwa kama tatizo linatambuliwa na kutibiwa haraka.

Lisipotibiwa husababisha viwango mbalimbali vya kupooza mwilini

Shinikizo la juu la damu, unene, wingi wa kolesteroli ya damu,  mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kisukari, chakula chenye mafuta mengi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kupatwa na kiharusi


Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children