SHINIKIZO LA DAMU
PRESHA (SHINIKIZO LA DAMU.
🩸Shinikizo la damu (Presha ) humaanisha nini?
Shinikizo la damu ni msukumo wa damu kwenye kuta za mishipa inayosafirisha damu.
🩸🩸🩸🩸🩸🩸🩸🩸
*Sababu za B.P*;
❇️Mara nyingi sababu ya watu wengi kupata tatizo la presha ya damu kuwa juu huwa hazijulikani.
Lakini kuna baadhi ya mambo huchangia presha ya damu kwa mtu kupanda kupita kiasi
1️⃣Umri mkubwa zaidi ya miaka 65 : Wazee huwa na presha ya juu kuliko vijana na watoto.
2️⃣Unene uliopitiliza.
3️⃣Kuwa na ndugu wa damu wenye matatizo ya presha
4️⃣Kuwa mazoea ya kutumia chumvi nyingi kwenye vyakula.
5️⃣Unywaji wa pombe kupinduika
6️⃣Kutopata usingizi wa kutosha nk.
Kumbuka Madhara ya kuishi na presha ya juu ya damu huwa ni makubwa.
Baadhi ya madhara ni pamoja na;
▶️Moyo kushindwa kufanya kazi
▶️Moyo kutanuka
▶️Shambulio la moyo
▶️Kiharusi
▶️Kuharibu figo na figo kushindwa kufanya kazi
▶️Kusababisha upofu
*NINI KIFANYIKE KUOKOA MAISHA NA KUEPUKA MADHARA HAYO* ?
⏺️Jenga utamaduni wa kupima presha watu wazima wenye umri kati ya miaka 18 hadi 39 wenye presha iliyo sawa, wasio na hatari yoyote ya kupata tatizo la presha hutakiwa kupima presha kila baada ya miaka 2 hadi 3. Watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea wenye kiwango cha presha kilicho sawa hutakiwa kupima presha kila mwaka.
⏺️Kula lishe nzuri hasa mboga za majani zaidi, nafaka zisizokobolewa, matunda.
⏺️Kupunguza uzito iwapo wewe ni mnene
⏺️Kuacha sigara iwapo unavuta sigara
⏺️Kupumzisha akili na kupunguza misongo ya mawazo.
⏺️Kupunguza kiwango cha chumvi unayotumia kwenye chakula
⏺️kufanya mazoezi
⏺️Dhibiti kiwango cha pombe iwapo unakunywa.
Comments
Post a Comment