Nimonia

 

Nimonia

Nimonia (kutoka Kiingereza"Pneumonia") ni hali ya kuvimba ya pafu—inayoathiri hasa vifuko vya hewa viitwavyo alveoli.[1][2] Husababishwa na maambukizi ya virusi au bakteria na kwa nadra kwa vimelea, baadhi ya dawa na magonjwa mengine kama ugonjwa wa kinga nafsia.[1][3]

Pneumonia
Mwainisho na taarifa za nje
An X-ray: showing a white wedge in the right lung field of a chest X-ray.
A chest X-ray showing a very prominent wedge-shape bacterial pneumonia in the right lung.
ICD-10J12.J13.J14.J15.J16.J17.J18.P23.
ICD-9480-486770.0
DiseasesDB10166
MedlinePlus000145
eMedicinetopic list
MeSHD011014

Dalili hasa ni kikohozimaumivu ya kifuajoto jingi mwilini na upumuaji mgumu.[4] vifaa vya utambuzi ni eksireina ukuzaji wa vimelea vya makohozi.

Chanjo za kuzuia baadhi ya aina za nimonia zipo. Matibabu hutegemea kisababishi cha msingi. Nimonia inayotazamiwa ya bakteria hutibiwa kwa antibiotiki. Iwapo nimonia hiyo ni kali, mwathiriwa hulazwa hospitalini.

Kila mwaka, nimonia huathiri takriban watu milioni 450  ambao ni asilimia saba ya idadi kamili ya watu duniani na husababisha takriban vifo milioni 4 . Ingawa nimonia ilichukuliwa na William Osler katika karne ya 19 kuwa "nahodha wa visababishi vya vifo",[5] majilio ya tiba ya antibiotiki na chanjo katika karne ya20yameendeleza kuongoka.[6]Hata hivyo katika nchi zinazostawi, na kwa wazee sana na wachanga sana na walio na wanaougua mara kwa mara, nimonia bado ndicho kisababishi kikuu cha vifo.[6][7]

Ishara and daliliEdit

Kiwango cha kutokea kwa dalili[8]
DaliliKiwango cha kutokea
Kikohozi
asilimia 79–91
Uchovu
asilimia 90
Kiwango cha juu cha joto
asilimia 71–75
Upungu wa pumzi
asilimia 67–75
maKohozi
asilimia 60–65
Maumivu ya kifua
asilimia 39–49
Mchoro wa mwili wa binadamu ukionyesha dalili kuu za nimonia
Dalili kuu za nimonia ya kuambukiza

Watu walio na nimonia ya kuambukiza mara nyingi huwa na kikohozi chenye kohozijoto jingi mwilini pamoja nabaridi inayotetemesha,upungufu wa pumzimaumivu ya kifua makali wakati wa kuvuta pumzi, na ongezeko la kiwango cha kupumua.[9] Kwa wazee, ishara inayoonekana sana inaweza kuwa kuchanganyikiwa.[9] Kwa watoto chini ya miaka mitano, ishara na dalili hasa ni joto jingi mwilini, kikohozi, upumuaji wa haraka au mgumu.[10]

Joto jingi mwilini si mahususi kabisa kwa sababu hutokea katika maradhi mengine mengi, na hali hii inaweza kukosa kwa walio na ugonjwa mkali sana auutapiamlo. Zaidi ya hayo, kikohozi hukosa mara nyingi kwa watoto wenye umri wa chini ya miezi miwili[10]Ishara na dalili zaidi kali ni:ngozi yenye rangi ya bluu kidogo, kiu kilichopungua, matukutiko, kutapika kunakoendelea, halijoto iliyopungua sana au iliyozidi sana, au kiwango kilichopungua cha fahamu.[10][11]

Visa vya nimonia ya bakteria na ya virusi hujitokeza kwa dalili sawa.[12]Visababishi vingine huhusishwa na sifa bainifu za kiafya zinazotokea sana bali zisizo maalum. Nimonia inayosababishwa na Legionella inaweza kutokea pamoja na maumivu ya fumbatio, kuhara, au kuchanganyikiwa,[13] ilhali nimonia inayosababishwa na Streptokokasi numoniae huhusishwa na makohozi yenye rangi ya kutu,[14] na nimonia inayosababishwa na Klebsiellainaweza kuwa na makohozi yenye damu ambayo mara nyingi huelezwa kama "jeli ya zambarau".[8] Makohozi yenye damu (yaitwayohemoptisisi) pia yanaweza kutokea katika kifua kikuu, nimonia isiyo na gram, usaha kwenye mapafu na aidha mara nyingi katikabronkitisi kali.[11] Nimonia ya maikoplasmainaweza kutokea kwa kuhusiana na kuvimba kwa tezi za shingomaumivu ya jointi, au maambukizi kwenye sikio la kati.[11] Nimonia ya virusi hujitokeza sana kwa kukoroma kuliko nimonia ya bakteria.[12]

VisababishiEdit

Vitu vitatu vya mviringo mmoja sehemu yake ya nyuma ikiwa nyeusi
bakteria sreptokokasi numoniae, kisababishi kikuu cha nimonia, ikionyeshwa kwa picha ya hadubini ya elektroni

Nimonia hutokana hasa na maambukizi yanayosababishwa na bakteria au virusina kwa viwango vidogo na kuvunaparasiti. Ingawa kuna zaidi ya aina 100 za ajenti za maambukizi zilizogunduliwa, ni chache tu zinahusika kwa vingi vya visa. Maambukizi yanayohusisha mchanganyiko wa virusi na bakteria yanaweza kutokea kwa hadi asilimia 45 ya maambukizi kwa watoto na asilimia 15 ya maambukizi kwa watu wazima.[6] Huenda ajenti inayosababisha isiweze kubainishwa katika takriban nusu ya visa licha ya kupima kwa makini.[15]

Wakati mwingine nenonimonia hutumika sana kwa ugonjwa wowote unaotokana na inflamesheni ya mapafu (inayosababishwa kwa mfano na magonjwa ya kinga nafsia, kuchomwa na kemikali au athari za dawa); hata hivyo kwa usahihi zaidi, inflamesheni hii huitwanimonitisi.[16][17] Ajenti zinazoambukiza zilikuwa zimegawanya kihistoria katika "za kawaida" na "zisizo kawaida" kwa msingi wa zilivyodhaniwa kujitokeza lakini ushahidi haujaunga mkono tofauti hii, kwa hivyo haitiliwi mkazo tena.[18]

Hali na visababishi vya hatari vinavyopelea nimonia ni: uvutaji, ukosefu wa kinga mwilini, ulevi ugonjwa sugu wa kufunga kwa mapafuugonjwa sugu wa figo, na ugonjwa wa ini.[11]Utumizi wa tiba zinazokandamiza asidi – kama vile kinza pampu ya protoni au H2 blockers- unahusishwa na ongezeko la hatari[19] ya nimonia. Uzee pia hupelekea nimonia.[11]

BakteriaEdit

Bakteria ndizo kisababishi kikuu cha nimonia iambukizayo katika jamii, ambapo Streptokokasi numoniaeilionekana kuhusika katika takriban asilimia 50 ya visa.[20][21] Bakteria zingine zinazohusika sana ni: Himofilasi influenzae katika asilimia 20, klamidofila numoniae katika asilimia 13, na Maikoplasma numoniae katika asilimia 3 ya visa;[20] Stafilokokasi aureasiMoraksela kataralisiLejionela numofilana Basili isiyo na gram.[15] Aina kadhaa za maambukizi yanayokinza dawa yaliyo hapo juu yamezidi kutokea sana, yakiwemo Streptokokasi numoniaekinzani na stafilokokasi aureasi-kinzani kwa methicillin.[11]

Ueneaji wa vimelea huendelezwa visababishi vya hatari vinapokuwa.[15]Ulevi unahusiana naStreptokokasi numoniaevimelea vya anerobi na Kifuakikuu cha maikobakteria; uvutaji huendeleza athari zaStreptokokasi numoniaeHimofilasi influenzaeMoraksela kataralisi, na Legionella numofila. Kutangamana na ndege kunahusiana na Klamidia sitasi; wanyama wa shambani na Kosiela baneti; aspiresheni ya vitu vya tumboni na vimelea vya anerobi; nayo faibrosi ya uvimbe na Seudomona erujinosa na Stafilokokasi aureasi.[15]Streptokokasi numoniae hutokea sana katika majira ya baridi,[15] na inapaswa kushukiwa kwa watu wanaopumua kiasi kikubwa cha vimelea vya anerobi.[11]

VirusiEdit

Kwa watu wazima, virusi huchangia takriban thuluthi moja[6] na kwa watoto taktiban asilimia 15 ya visa vya nimonia.[22] Ajenti zinazoshukiwa sana ni: virusi vya rainovirusi vya koronavirusi vya influenza,virusi vya kupumua vya sinsitiavirusi vya adeno, na [[virusi vya parainfluenza].[6][23] Virusi vya hepesi simpleksi havisababishi nimonia sana, isipokuwa kwa vikundi kama vile: watoto wachanga, watu walio na saratani, waliopokea ogani za mwili, na watu walio na majeraha makubwa ya moto.[24] Watu waliopokea ogani au wale ambao kwa njia nyingine miili yao imepoteza uwezo wa kujikinga na maradhi huwa na viwango vikubwa vya nimonia ya virusi vya kuvimba kwa seli`.[22][24] Walio na maambukizi ya virusi wanaweza kuambukizwa tena na bakteriaStreptokokasi numoniaeStafilokokasi aureasi, au Himofilasi influenzae, hasa panapokuwa na matatizo mengine ya kiafya.[11][22] Virusi tofauti huzidi katika vipindi tofauti vya mwaka, kwa mfano katika msimu wa influenza, influenza inaweza kuchangia zaidi ya nusu ya visa vyote vya virusi.[22]Milipuko ya virusi vingine pia hutokea mara chache, vikiwemo virusi vya hantana virusi vya korona.[22]

KuvuEdit

Nimonia ya kuvu haitokei sana, lakini hutokea sana kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kingamwili kutokana naUKIMWI, [dawa zinazozuia utendaji kazi wa kingamwili]], au matatizo mengine ya kiafya.[15][25] Mara nyingi husababishwa na Histoplasma capsulatum, blastomaisesi, Kryptokokasi niofomaniNumosisitisi jirovesi, na Koksidiodi imitisiHistoplasmosisihutokea sana katika Bonde la mto wa Mississippi, na koksidioidomikosihutokea sana katika Kusini magharibi mwa Marekani.[15] Idadi ya visa imekuwa ikiongezeka katika nusu ya mwisho ya karne ya 20 kutokana na ongezeko la usafiri na viwango vya ukandamizaji kinga kwa watu.[25]

ParasitiEdit

Aina tofauti za parasiti zinaweza kuathiri mapafu, zikiwemo: Toxoplasma gondiiStrongiloidi stakoralisi,Minyoo mviringo, na Plasmodiamu malariae.[26] Vimelea hivi huingia mwilini kupitia mgusano wa moja kwa moja wa ngozi, kumeza au kupitia mdudu ambaye ni vekta.[26]Isipokuwa Paragonimasi westamani, parasiti nyingi haziathiri mapafu hasa, bali huhusisha mapafu baadaye baada ya sehemu zingine.[26]Parasiti zingine, hasa zile za jenera ya mnyoo wa Askaris naStrongiloidihuchochea mwitiko mkali wa esinofili, ambao unaweza kusababisha nimonia ya kiesinofili.[26] Katika maambukizi mengine, kama vile malaria, kuhusika kwa mapafu hutokana hasa na inflamesheni inayochochewa na saitokini.[26] Katika ulimwengu uliostawi, maambukizi haya hutokea sana kwa watu wanaorudi kutoka safarini au kwa wahamiaji. [26] Dunani kote, maambukizi haya hutokea sana kwa wasio na kingamwili.[27]

Yenye asili isiyojulikanaEdit

Nimonia ya tishu za mapafu yenye asili isiyojulikana au nimonia isiyoambukiza[28] ni aina yaugonjwa wa mapafu unaosambaa. Nao ni: uharibikaji unaosambaa wa alveolasinimonia ya organizingnimonia ya tishu za mapafu isiyo dhahirinimonia ya limfosaiti ya tishu za mapafunimonia ya kupukutika kwa tabaka la juu la tishu ya epithelia ya mapafuugonjwa wa kupumua wa bronkiolitisi wa tishu za mapafu, na nimonia ya kufanyika kunakoendelea kwa kovu kwenye tishu za mapafu.[29]

UzuiajiEdit

Uzuiaji huhusisha uchanjaji, hatua za kimazingira na matibabu yafaayo ya matatizo mengine ya kiafya.[10]Huaminika kuwa kama hatua zinazofaa za uzuiaji zingekuwa zimeanzishwa kote ulimwenguni, vifo vya watoto vinaweza kupunguzwa kwa 400,000 na kama matibabu yafaayo yangepatikana kwa wote, vifo vya utotoni vinaweza kupunguzwa kwa vifo 600,000 zaidi.[12]

UchanjajiEdit

Uchanjaji huzuia dhidi ya nimonia fulani za bakteria na za virusi kwa watoto na watu wazima. Chanjo ya influenza ni bora dhidi ya influenza A na B.[6][45]Taasisi ya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa imependekeza uchanjaji wa kila mwaka kwa kila mtu aliye na umri wa miezi 6  na zaidi.[46] Kuwapa wahudumu wa afya kingamaradhi hupunguza hatari ya nimonia ya virusi miongoni mwa wagonjwa wao.[41]Milipuko ya influenza inapotokea, dawa kama vile amantadine aurimantadinezinaweza kusaidia kuzuia ugonjwa huo.[47] Haijulikani kama zanamivir au oseltamivir ni bora kwa sababu kampuni inayotengeneza oseltamivir imedinda kutoa data ya majaribio kwa uchanganuzi wa kibinafsi.[48]

Chanjo dhidi ya Hemofilasi influenzae na Streptokokasi nimoniae zina ushahidi dhabiti wa kuunga mkono matumizi yake.[30] Kuwapa watoto chanjo dhidi ya streptokokasi numoniae kumepelekea kupungua kwa visa vya maambukizi haya kwa watu wazima kwa sababu wengi wao hupata maambukizi kutoka kwa watoto. Chanjo ya Streptokokasi nimoniae ya watu wazima ipo na imeweza kupunguza hatari ya ugonjwa vamizi wa numokokasi[49] Chanjo zingine zinazokinga dhidi ya nimonia ni: kifadurotetekuwanga, na ukambi.[50]

NyingineEdit

Kusitisha uvutaji wa sigara[37] na kupunguza uchafuzi wa hewa vyumbani, kama vile kupika kwa kuni vyumbani ausamadi, yote yamependekezwa.[10][12]Uvutaji wa sigara unaonekana kuwa ndicho kisababishi kikuu cha nimonia ya numokokasi kwa watu wazima wenye afya. [41] Usafi wa mikono na kukohoa kwenye mkono wa nguo kunaweza pia kuwa njia bora ya uzuiaji.[50] Uvaaji wa barakoa za upasuaji kwa walio wagonjwa pia unaweza kuzuia maradhi.[41]

Kutibu maradhi fiche (kama vile VVU/UKIMWIkisukari melitasi, na utapiamlo) ipasavyo kunaweza kupunguza hatari ya nimonia.[12][50][51]Kwa watoto wa umri wa chini ya miezi 6 kunyonya bila kupewa chakula kingine chochote hupunguza hatari na ukali wa ugonjwa.[12] Kwa walio na VVU/UKIMWI na idadi ya CD4 chini ya seli 200 kwa kila uL, antibiotiki iitwayo trimethoprim/sulfamethoxazolehupunguza hatari ya Nimonia ya numosisitisi[52]huenda ikawa ni ya kufaa kwa walio na kingamwili dhaifu lakini wasio na VVU.[53]

Kuwachunguza wanawake wajawazito kwa Streptokokasi ya kundi B na Klamidia trakomatisi, na kutoa matibabu kwa antibiotiki, ikihitajika, hupunguza viwango vya nimonia kwa watoto wachanga;[54][55] mbinu za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto huenda zikafaa pia.[56]Efusheni ya mdomo na koo la watoto wachanga waliochafuliwa kwa kiowevu cha amnioni chenye mekoniamu haijaweza kupunguza kiwango cha nimonia ya aspiresheni na huenda ikasababisha madhara,[57] hivyo basi, tendo hili halipendekezwi katika hali nyingi.[57] Kwa wazee wadhaifu, huduma nzuri ya afya ya mdomoni inaweza kupunguza hatari ya nimonia ya aspiresheni.[58]

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children