FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA KIHARUSI

 UGONJWA WA KIHARUSI : MAMBO MUHIMU KUFAHAMU

Maana

Kiharusi ni ugonjwa wa dharura na hatari ambao hutokea pale seli za ubongo zinapokufa kwa kukosa hewa ya oksijeni na chakula kutokana na kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.

Aina za kiharusi

Kuna aina kuu mbili za Kiharusi

  1. Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo
  2. 2. Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo

Ukubwa wa tatizo la kiharusi

1. Kiharusi ni muuaji namba 2: Kwa mwaka 2015 kulingana na ripoti maalumu ya Shirika la Afya duniani WHO kuhusu sababu za vifo ilionesha kiharusi kinashika nafasi ya pili kati ya magonjwa yote kwa kusababisha vifo vingi.

2. Kiharusi husababisha ulemavu kwa wengi: Kiharusi kinashika nafasi ya tatu kati ya visabibishi vya ulemavu duniani. Waathirika wengi huishia kuwa walemavu

Dalili za kiharusi

1.GANZI

-Mtu anayepata kiharusi hupata ganzi inayoanza ghafla na mara nyingi huathiri upande mmoja wa mwili. Mfano: Upande mmoja wa uso kufa ganzi na kushindwa kuongea vizuri au kutabasamu

2.KUPATA SHIDA KUONGEA

Mgonjwa wa kiharusi hushindwa kuongea vizuri, utoaji wa maneno huwa sio wa kawaida

Mfano: Mgonjwa kushindwa kumaliza sentensi au kuongea kama amelewa sana

-Pia hali hii huweza kuambatana na kutoka mate(udenda) kwa wingi mdomoni

3.Kushindwa kuona

Mgonjwa wa kiharusi anaweza kushindwa kuona, hali hii hutokea ghafla. Inaweza kuhusisha jicho moja au macho yote mawili.

4.Pia mgonjwa anaweza kupoteza fahamu au kupata degedege

5. Mgonjwa anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa au ndogo au vyote viwili

VITU VINAVYOCHANGIA MTU KUPATA KIHARUSI

1. Ugonjwa wa Shinikizo kubwa la damu (presha)

2. Uvutaji sigara

3. Ugonjwa wa kisukari

4. Magonjwa ya moyo hasa ugonjwa wa mtetemo wa moyo (atrial fibrillation)

5. Tatizo la mafuta mengi kwenye damu (Lehemu au cholesterol)

6. Uzito uliopitiliza

7. Unywaji wa pombe uliokithiri

8. Kutokufanya mazoezi

GUNDUA KIHARUSI HARAKA UOKOE MAISHA YA MPENDWA, NDUGU AU JAMAA

Kiharusi ni tatizo la dharura linaloweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kifo au ulemavu kama mtu asipopata matibabu mapema. Hivyo ni vyema kila mtu akafahamu dalili za kiharusi ili iwe rahisi kuzitambua. na kuchukua hatua mapema.

Ili kurahisha kumbukumbu za dalili za kiharusi kifupisho FAST (Face Arm Speech Time) hutumika kama ifuatavyo

Face (Uso)

-Angalia kama upande mmoja wa uso uko tofauti na mwingine. Mwambie mgonjwa. anyanyue kope au akunje ndita au atabasamu. Upande ulioathrika utashindwa kufanya hivyo.

Arm. (Mkono)

Mwambie mgonjwa anyanyue mikono juu kwa mbele au juu mara nyingi mkono wa upande ulioathirika hushindwa kunyanyuka au hudondoka unaporudishwa chini.

Speech (Uongeaji)

Mwambie mgonjwa atamke jina lake, mtu mwenye kiharusi hushindwa kuongea, au huongea kama. mlevi au hupata shida kutafuta maneno kama mtu aliyepoteza kumbukumbu

Time (Muda)

Muda ni mali, chukua maamuzi ya kutafuta msaada wa kitabibu haraka maana kadri unavyochelewa ndio kiharusi kinaharibu sehemu muhimu za ubongo

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI