UGONJWA WA AMIBA

GONJWA WA AMIBA


Huu ni ugonjwa unaosababiushwa na Wadudu wanaojulikana kama entamoeba Histolytica.wadudu hawa wanapatikana kwenye kinyesi cha binadamu alien a ugonjwa huu na huingia tumboni mwa mtu mwingine baada ya kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye wadudu hawa.

WATU GANI WAKO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU
Ugonjwa huu upo sana kwenye nchi zinazoendelea san asana katika bara la ASIA,America ya kati,Africa na Amerika ya kusini.Takwimu zinasema kwamba takiribani watu  millioni 500 Duniani hupata ugonjwa huu kila mwaka,na watu 500 hufa kutokana na ugonjwa huu kila mwaka.

  • Watu walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu ni kama ifatavyo
  • Watu wanaoishi kwenye mazingira yasiyo safi
  • Watu wanaotumia maji yasiyo safi na salama
  • Watu wanaoishi mazingira yenye msongamano wa watu na maeneo kama magereza.
  • Watu wenye kinga duni mfano watu wenye UKIMWI
  • Watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile


NINI HUSABAISHA UGONJWA HUU
Entamoeba histolytica ni mdudu anaesababisha ugonjwa huu.Wadudu hawa huingia mwilini pale mtu anapokula mayai(cysts) ya wadudu hawa kupitia chakula au maji yalichafuliwa au kupitia mikono iliyochafuliwa na mayai ya wadudu hawa. Mayai ya wadudu hawa huweza kuishi kwa muda miezi 5 bila kuharibika kwenye udongo au chakula.
Mayai haya yanapoingia kwenye tumbo na utumbo hujishikiza kwenye kuta za utumbo na kuanguliwa kutoa aina ya wadudu hawa inayojulikana kama trophozoites,Hapa wadudu wanazaliana na kuchimba kuingia ndani ya kuta za utumbo hali inayopelekea mtu kuhara choo chenye damu,maumivu ya tumbo na saa nyingine kusababisha uvimbe kwenye utumbo(ameoboma) .Mtu mwenye ugonjwa huu hujisaidia kinyesi chenye mayai (cysts) ya wadudu hawa.
Pia wadudu hawa wanaweza kuingia kwenye mzunguko wa damu na kusafiri kwenda maeneo mbali mbali ya mwili kama ubongo,Ini,Figo na kuleta madhara.Asilimia kubwa huenda kwenda Inni ambapo husababisha ini kutunga usaa( Amoebic liver absess)

Related image

DALILI ZA AMIBA
Dalili huanza kuonekana ndani ya week 1 hadi 4 tokea mtu amekula mayai ya wadudu hawa.Dalili za ugonjwa huu ni
  • 1.       Maumivu ya tumbo ,Ambapo tumbo linakua kama linanyonga na maumivu yanakua hasa sehemu ya kitovu.
  • 2.       Kuhara choo kilichochanganyikana na vitu vinateleza kama kamasi na saa nyingine kimechanganyikana na damu
  • 3.       Kuhisi haja na ukienda chooni unapata choo kidogo sana
  • 4.       Tumbo kujaa Gesi

Endapo wadudu wameathiri  Ini mtu hupata dalilia kama
Homa
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya tumbo hasa sehemu ya kulia ya tumbo karibu na kifua.
Image result for amoebic liver abscess
VIPIMO
Ugonjwa huu upimwa kupitia kupima kinyesi ili kuangalia wadudu hawa na mayai (cyst) yao.Pia unaweza kupima vipimo vya kuangalia ini kama limeathirika na ugonjwa huu pia.

MATIBABU
Ugonjwa huu hutibiwa na dawa katika kundi la dawa za antbiotics ambazo ni METRONIDAZOLE(FRAGYL)  pamoja na tinidazole. Endapo wadudu hawa wamesababisha madhara makubwa kwenye utumbo mfano kutoboa utumbo basi mtu huitajika kufanyiwa upasuaji.
MUHIMU: UONAPO DALILI HIZO FIKA HARAKA HOSPITAL UPATE VIPIMO NA MATIBABU.

JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
Usafi wa mazingira,maji na chakula ndio njia kubwa ya kukukinga na ugonjwa huu,ikihusisha kunawa mikono kwa maji safi na sabuni unapotoka chooni.Vitu vingine vya kuzingatia ni pamoja na


  • Kuosha vizuri matunda na mboga mboga kabla ya kula
  • Epuka kula matunda na mboga mboga ambazo hujaziosha wala kuzimenya wewe mwenyewe
  • Chemsha maji ya kunywa au tumia maji yaliyo salama mfano yaliyowekewa dawa ya chlorine(water guard)
  • Epuka kutumia maziwa au bidhaa za maziwa kama Cheese ambayo hayajachemshwa vizuri
  • Kama ni mpenzi wa Kchumbali au Salad kwa kuwa hazipikwi  weka VINEGAR kwani mbali na kuweka radha ya uchachu ila ina ACETIC ACID ndani yake ambayo husaidia kuua wadudu.

Ugonjwa wa amiba sio wa kuchukulia poa kwani usipotibika mapema huweza kuleta madhara makubwa sehemu mbalimbali za mwili. Ni vyema kuzingatia usafi wa mazingira maji na vyakula ili kuepuka hatari ya kupata ugonjwa huu.na unapopata dalili hizo basi wahi hospitali kupata matibabu

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip