Kifafa cha Mimba

Kifafa cha Mimba baada ya kujifungua

Mimba inakuja na matatizo mbalimbali ya kiafya. Mengi yanaondoka baada ya kujifungua, na mengine yanabaki kwa mda mrefu. Ubaya ni kwamba kuna baadhi yanazaliwa baada ya kujifungua kama kifafa cha mimba baada ya kujifungua.

Hali hii inahitaji matibabu ya haraka maana inaweza sababisha mshtuko wa moyo na matatizo mengine ya kiafya hasa kwa wamama wapya.

Kifafa cha mimba baada ya kujifungua ni nini?

Kifafa cha mimba hutokea wakati wa ujauzito. Shinikizo kubwa la damu na uwepo wa protini katika mkojo (zaidi ya 300mg) inasababisha kifafa cha mimba mara baada ya kujifungua.

Hali hii inaweza kuchukua zaidi ya masaa 48, ikiwa umebainika umepata kifafa cha baada ya kujifungua,unaweza kubaki hospitali mda mrefu zaidi mpaka shinikizo la damu litakapopungua. Ikiwa itaendelea matibabu yatahitajika kudhibiti hatari za mishipa ya moyo inayoweza kupelekea matatizo ya moyo na  mishipa ya damu milele.

Dalili na ishara za kifafa cha mimba

Ni ngumu kutambua kifafa cha mimba. Mara nyingi wanawake wanaweza wasionyeshe dalili zozote za kifafa cha mimba wakati wa ujauzito.

Hizi ni  baadhi ya dalili :

Shinikizo kubwa la damu(kipimo kinaonyesha 140/90 au juu zaidi)

Zaidi ya 300mg ya protini kwenye mkojo

Kushindwa kuona vizuri kwa mda mfupi. Shinikizo la damu linafanya macho kuwa nyeti sana kwenye mwanga.

Kuongezeka uzito haraka sana

Miguu na uso wako kuvimba

 

Chanzo cha kifafa cha mimba

Chanzo sahihi cha tatizo hili hakijulikani. Kifafa cha mimba kinaweza kuanza kabla ya kujifungua, ila kikaonekana baada ya kujifungua. Ikiwa kuna historia ya tatizo hili katika familia yenu, basi uko hatari kupata tatizo hili.

Vitu hatarishi vinavyohusiana na kifafa cha mimba

Nafasi yako ya kupata kifafa cha mimba itaongezeka kama:

Shinikizo la damu linakua baada ya wiki ya 20 ya ujauzito

Umepata ujauzito kabla ya miaka 20 na baada ya miaka 40.

Kama mama yako au ndugu yako katika familia ana rekodi ya kuwa na ugonjwa huu.

Una uzito mkubwa

Una ujauzito wa mapacha au watoto zaidi.

Utambuzi wa kifafa cha mimba

Mara baada ya kujifungua,daktari atakuangalia shinikizo la damu kabla ya kuruhusiwa hospitalini. Ikiwa daktari atahisi una kifafa cha mimba, atakuagiza ufanye vipimo vya damu na mkojo.

Kipimo cha damu:

Kipimo cha damu kitaangalia ufanyaji kazi wa ini na figo, pia inachunguza chembechembe za kugandisha damu kama zimepungua kuliko kawaida. Ni muhimu kujua namba ya chembechembe za kugandisha damu kwasababu seli hizi zinazuia damu kuganda na kutokwa damu kupindukia.

Kipimo cha mkojo:

Kipimo hichi kinafanyika kujua kiasi cha protini katika mkojo. Kama kiwango cha protini ni kikubwa kwenye mkojo, inaweza kuonyesha una kifafa cha mimba. Kama kipimo chako ni chanya, utashauriwa kuendelea kukaa hospitali zaidi kutibu hali hii kwa matibabu sahihi.

Matibabu ya kifafa cha mimba

Ikiwa imebainika una kifafa cha mimba, daktaria atapendekeza matibabu ya kutibu shinikizo la damu. Katika kifafa cha mimba kidogo daktari atasimamia upatiwe magnesiam sulphate kwa masaa 24. Utaangaliwa kwa karibu na daktari wako kwa dalili zozote za kifafa cha mimba. Vipimo vya shinikizo la damu na mkojo vitachukuliwa pia. Utapatiwa dawa za kuweka shinikizo la damu katika hali ya kawaida kama shinikizo ni zaidi ya 150/100.

Jinsi ya kuepuka kifafa cha mimba

Hakuna njia zijulikanazo za kuepuka kifafa cha mimba. Ingawa kuangalia afya yako inaweza kufanya mabadiliko. Zifuatazo ni njia zinazoweza kukusaidia:

Dhibiti uzito wako kwa kula vizuri na kufanya mazoezi. Uzito mkubwa au uzito duni unakuweka katika hatari za kupata tatizo.

 

Kula vizuri, vyakula vyenye vitamin na madini ili kukusaidia kudhibiti shinikizo la kawaida la damu kipindi chote cha ujauzito.

Kunywa maji ya kutosha na maziwa ili kuwa na maji mengi mwilini. Acha kahawa na pombe.

Mtembelee dakatri wako kipindi cha ujauzito ili ufanyiwe vipimo vya damu na mkojo kuchunguza kama kuna kifafa cha mimba katika hatua za awali.

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip