Vitu vya kuacha ili uweze kufanikiwa zaidi katika miezi 12 ijayo

 



Vitu vya kuacha ili uweze kufanikiwa zaidi katika miezi 12 ijayo 



#1.acha kuwa na udhuru “excuses” wa kushindwa kufanikisha mipango yako

Nimetokea katika familia ya kati, Skua na ajira wala mtaji, Ilifikia hatua nika kaa chini na kujiuliza nitaendelea kuweka udhuru mpaka lini, ni lini nitaanza kufanya ninachotakiwa kufanya ili nifanikiwe maishani? Niliamua kuzingatia zaidi “kufokas” kwenye vitu ambavyo ninaweza kuvifanya ili nibadili maisha yangu na nikaacha kuangalia changamoto gani zina nizonga katika maisha

Asilimia 99 ya vijana wanashindwa kutoboa maishani kwa sababu ya kuweka udhuru, Utasikia “ah serikali hii haitujali” mara “aah sina connection” “wazazi wangu ni maskini” uchumi wan chi yetu ni mbovu”   “hali ya hewa”

Ukweli ni kwamba ukitafuta udhuru ( au vijisababu ) utapata sababu za kutosha kwa nini hutwezi kufanikiwa   

Amua nini unakitaka na uanze kukifanya sasa hivi haijalishi ita kughalimu nini


#2. Acha kujilinganisha na wenzio

Kuishi kama wewe kwenye dunia ambayo inataka uwe kama inavyotaka ni kitu kikubwa sana maishani. Usitake kua kama walimwengu wanavyo taka, usijaribu kujilinganisha na Fulani.

Watu wengi wameathiriwa na kitu kinachoishwa “social proof” yaani  kufanya vitu Fulani kwa sababu wengine wanafanya. Mwingine anasoma kozi ya afya kwa sababu wengi wanasoma, mwingine anaende sehemu Fulani kwa sababu watu wote wanaenda huko.

Albert Einsten alisema “uki muhukumu samaki kwa sababu ya uwezo wake wa kupanda mti, ataishi maisha yake yote akiamini ni mjinga” . Watu wengi hawajikubali na kujiamini si kwakua si wazuri ila ni kwa sababu wanajilinganisha sana na watu wengine”

Acha kujilinganisha na wengine , Jijue wewe ni nani na unataka nini katika maisha yako, na pambana kuwa bora zaidi ya jana 

Samaki hana sababu ya kupanda mti, kobe hana haja ya kukimbia kama farasi. Utapata mafanikio zaidi katika maisha kama uki pambana kuwa bora zaidi ya jana, acha kujilinganisha na watu

#3. Acha kupoteza mda

Niliamka siku moja na kuamua kufuta mtandao wa kijamii “wa instagram “  kwenye simu yangu , rafiki zangu walinishangaa, lakini kuna kitu kilinifanya nifanye hivyo, 

Niligundua kua napoteza lisaa limoja kila siku niki peruzi kwenye mtandao huo

Kama ukijifunza ujuzi flani kwa saa moja kila siku, baada ya miaka mitano , utakua mtaalamu nguli  wa kimataifa katika ujuzi huo unaojifunza  , hii inamaanisha kama nikiutumia muda wa lisaa limoja ninao upoteza kwenye mtandao wa kijamii katika fani yangu kwa miaka mitano nitakua mtaalamu katika fani yangu

Henry ford alisema “nimegundua kua watu wengi wanarudi wanasonga mbele wakitumia muda uleule,ambao wengine wanaupoteza”

Kila binadamu ana masaa 24, tatizo watu wengi tuna poteza mali ya thamani tuliyo nayo ambayo ni muda, Muda unaoupoteza ndio uleule ambao wenzako wanautumia kupata maarifa yatakayo wasaidia kufanikiwa zaidi maishani

Benjamin Franklin alisema “muda ni pesa”

#4. Acha kutegemea mtaji mkubwa

Rafiki angu mmoja alikuja ofisini kwangu na mpango wa kibiashara “business plan”  ambao unahitaji milioni tatu ili kuutekeleza , wakati huo hajawai kuendesha biashara ya aina yoyote ile . Niliangalia mpango wake wa kibiashara na kupunguza kiwango cha pesa mpaka laki tano. Nilimwambia “kama huwezi kuanza na kidogo huwezi kuanza kabisa”

Watu wengi wanatamani kuanzisha biashara zao lakini wanataka kuanza na mamilioni ya pesa   kabla hawajaweza kuanza . “ooh pole rafiki yangu” kama huwezi kuanza na kidogo basi huwezi kuanza kabisa 

Kama unataka kutimiza ndoto yako unatakiwa uanze na chochote kile ulicho nacho  , hapo hapo ulipo 

#5. Acha kutegemea ramani ya kukuongoza 

Miaka kumi iliyopita nilipo ingia kwenye biashara kitu cha pekee nilicho kua na kijua ni kile nilicho kua nakihitaji yaani “uhuru wa kiuchumi”, sikujua ni jinsi gani nitapata uhuru huo , wala sikujua ni nini nitafanya , niliamua tu kutoka na kuamini ntajua kila kitu njiani

Watu wengi wanaamini lazima kuwe na ramani , wanakua na mashaka ya kuanza kwa kua hawajui wataanzia wapi na wataishia wapi

Maisha hayana ramani, unatakiwa utoke , chafuka mikono na kila kitu kitajipanga utakapo kua unaendelea na safari

#6.Acha kukosa “imani”

Muhaman Ali alisema “ni kukosa imani kunakofanya   watu waogope kupambana na changamoto”

Nakupa changamoto hii “usitegemee ramani wala kujua kila kitu katika safari ya mafanikio yako”, sababu inayowafanya watu wasubiri “ramani” ni kukosa imani 

Imani ni uhakika kile ambacho hujaona, kama unajiamini na unamwamini Mungu Utatoka bila ya ramani wala muongozo, kwa sababu una imani njia itafanyika, 

Jiamini na amini nguvu ulizo nazo, nenda na ufanye mambo yatokee

#7. Acha kutegemea watu wakutendee wema

Nimekua nikisikia watu wakiwalalamikia waajiri wao, wanalala mikia wanasiasa, serikali, wazazi, na wapenzi wao

Sababu inayokufanya wewe ulalamikie watu hao ni kwa sababu una tegemea watu hao wakutendee mema “oh pole” ni hatari sana kutegemea watu wakutendee wema, kwakua watu wengi si wema hahahahaha

Kama unataka kuwa na mafanikio maishani jifunze kuishi bila kutegemea huruma ya mtu yeyote, kwa sababu utakapo kua unategemea huruma ya watu wengine, mshahara wa watu wengine, au kutegemea mtu flani akupe mahitaji yako, flani awe mpole kwako . Mtu huyo atakuumiza.

#8. Acha kutegemea muujiza toka kwa serikali 

Serikali haitatui matatizo “huyaficha tu”

Serikali haitatui matatizo “inayaongelea tu”

Acha kutegemea muujiza toka kwenye serikali chukua  jukumu lote la maisha yako, na utakua na mafanikio zaidi katika maisha.

# usiogope kushindwa

Nina taarifa nzuri, oh kiukweli ni taarifa mbaya kuna nyakati “utashindwa” “utaanguka” 

Haialishi unaogopa kiasi gani kushindwa ama ni mpambanaji usie ogopa, kuna nyakati utashindwa katika harakati zako za kutafuta mafanikio

Mafanikio ni kwa wale watu ambao wanaweza wakavumilia kushindwa, wale ambao haijalishi wanaanguka marangapi lakini wanainuka na kuendelea na safari

Fanya unachotakiwa kufanya bila kuhofia utashindwa, tatua c 

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip