Maamuzi magumu yakuchukua unapoanza mwaka 2021

Maamuzi magumu yakuchukua unapoanza mwaka 2021
Mwaka unapoanza ni muda wa kuweka mipango na mikakati ya kufanikiwa zaidi kuliko mwakajana
Naongelea kufanikiwa kiuchumi hasa, na pia kijamii na kadhalika, ni wakati wa kufanikiwa zaidi.
Maamuzi ya kweli ni magumu na ndio sababu watu wengi wanashindwa kuyafanya,
Leo nitakwambia kuhusu maamuzi matatu ambayo ukiyachukua kwa mwaka mpya wa 2021 yanaweza kukusaidia kufanikiwa kiuchumi kijamii na kadhalika
# 1. jifunze kuhusu watu walio fanikiwa
Sisi sote tunao watu ambao tunawaamini na kuwaheshimu, hao ni watu walio fanikiwa katika mambo mengi katika maisha yao, 
Jifunze maisha ya watu waliofanikiwa, jifunze kuhusu wajasiria mali wakubwa, wanasiasa na wanasiasa wakubwa duniani mfano Tomas Edison, Newton na  Steve Jobs
Jifunze kipindi cha maisha yao kabla hawajafanikiwa , 
Watu hao walitokana na maisha magumu kabla hawajafanikiwa, Kujifunza kuhusiana na watu hao changamoto walizopitia na namna walivyo kabiliana nazo itakupa uwezo wa kufanikiwa katika vitu unavyotaka kufanikisha
#2 Fanya vitu ambavyo huna uhakika kama vitafanikiwa
Nilipo ingia kwenye ujasiriamali miaka nane iliyopita sikua na uhakika kama nitafanikiwa, vikwazo vilikua vingi
Lakini kitu kama ni muhimu sana fanya usijali changamoto
Watu wengi wanashindwa kuanza kufanya biashara kwa kuogopa kua hawana mtaji, wengine wanasema kua hawana fedha, 
Unapoanza mwaka kaa chini na kiulize ni kitu gani huwa unataka sana kufanya lakini una ogopa , Kitafute kitu icho na anza kukifanya, ni kweli utapata changamoto na uta feli wakati mwingine lakini jaribu tena na tena bila kukata tama, hatimaye utafanikiwa

#3 amua kua mesia unae msubiri

Mara nyingi nawasikia watu wakilalamika mda wote kuhusu hali ya kukosa ajira, kukosa fursa, kukosa mkopo, na wanalala mikia saana wana siasa

Kila mtu analalamika anataka serikali na mwanasiasa wawe mesia wa kumuokoa toka kwenye changamoto ya ajira na umasikini

Lakini najiuliza kwa nini wote tusiamue kutatua changamoto zetu, kwanini tusiwe mesia tunae mtafuta tujiokoe na hali ngumu.

Tuamue mwaka huu kutatua matatizo yetu, tuamue  kushughulikia umasikini na tatizo la ajira sisi wenyewe,

Huna mtaji ? hilo ni tatizo kwa wengi, anza na nguvu zako huo ndio mtaji mkubwa ulio pewa, una ubongo kiungo cha pekee, una mkono mguu, una ardhi au unaweza kukodi, una uhai  una afya .  una taaluma, una watu wanao kupenda. anza na  ulicho nacho 

Je ni mwalimu anza na taaluma yako, anza kujitolea, jaribu mikopo, jaribu kilimo, jaribu kibarua chochote jaribu njia  zote unazoweza kuzitumia cha msingi usikae tu na kusubiri muujiaza, ama mtu Fulani aje akuokoe toka kwenye matatizo yako kwa sababu hata tokea. Amua kua mesia unae muongelea

Ni njia ngumu sana na ni vigumu sana kupita njia hii, lakini kama utaweza utashukuru baadae, utaweza kuwasaidia wengine

Amua kutatua matatizo machache kati ya unayo lala mikia

Comments

Popular posts from this blog

KOZI YA KOMPYUTA KWA KISWAHILI

Lies the poor parent tell children