JINSI YA KUTENGENEZA MEMORI KADI AU FLASHI ILIYO HARIBIKA / KULIWA NA VIRUS

  JINSI YA KUTENGENEZA MEMORI KADI AU FLASHI ILIYO HARIBIKA / KULIWA NA VIRUS



 Kuaribika kwa flashi ni kitu kinachoumiza sana lakini kuna mbinu unaweza kujaribu kuzitumia ili kuirejesha katika hali yake . Tumia kompyuta yako unapotumia mbinu hii Tumia nyezo “tool” inayoitwa “command prompt” au kwa kifupi cmd , kw akutumia mbinu hii unatakiwa unandike maelekezo “commands” ili uweze kufomati memori au flashi iliyo haribika  Fuata hatua zifuatazo 

1. Chomeka flashi iliyo haribika au kuliwa na virus

 2. Peleka kielekezi cha mouse “pointer” kwenye batani ya mwanzo “start button” na ubonyeze bofye mouse kitufe cha kulia “right click” au nenda sehemu iliyoandikwa “search” na uandike CMD alafu ubofye, kidirisha cmd “cmd window” kitatokea

 3. Adnika “diskpart”  alafu bofya kitufe kilichoandikwa “enter”

 4. Andika “list disk” alafu bofya “enter” utaona mlolongo wote wa vitunza taarifa “storage devices” kwenye kompyuta yako 

5. Andika “select< namba ya disk yako> na ubonyeze “enter” kwa mfano “select disk 1” 

6. Andika “clean” alafu bofya “enter” 

7. Andika “ create partition primary” alafu  “enter”

 8. Andika “active “ alafu “enter”

 9. Andika “select partition 1” 

10. Andika format fs=fat32 alafu “enter”  

Mchakato wa kuformat utaanza, una weza andika “ntfs” badala ya fat 32 kama una flashi kubwaw inayozidi GB 4 , usifunge CMD 

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip