Njia tatu zitakazo kusaidia ili uweze kuuza zaidi

 Njia tatu zitakazo kusaidia ili uweze kuuza zaidi 



Ujasiriamali si tu kutengeneza bidhaa  au huduma bora kwa ajili ya watu , Ili uweze kufanikiwa zaidi katika ujasiria mali ni vyema uwe na uwezo zaidi wa kuuza bidhaa au huduma yako Ufanye nini ili watu waweze kununua kwako zaidi kuliko kwa watu watu wengine walio katika soko lako Zifuatazo ni mbinu tatu ambazo kama ukizifuata zitakusaidia uweze kuuza zaidi bidhaa au huduma zako za ujasiriamali katika soko

 #1. Wapende watu

   Ili watu waweze kupenda na kununua bidhaa yako, waweze kusema ndio ni vizuri kujua saikolojia ya kushawishi , Ili kumshawishi mtu kirahisi ni vizuri zaidi ukamfanya akupende wewe kwanza. Binadamu hatupendi mtu anapotulazimisha kununua ,

  Kama nikikupenda nitakuamini na nikikuamini itakuwa rahisi kwangu kufungua waleti yangu na kununua kwako. Ili wateja wakupende ni muhimu uwapende kwanza, hutakiwi kuigiza kwa kua ukiigiza wateja watagundua Ukichukia tatizo unalo litatua itakua rahisi kupenda utatuzi ambao unaletwa na bidhaa au huduma unayo itoa, Steve Jobs alipendwa kwa kua alikua anachukia jinsi kompyuta ilivyokua inapatikana kwa watu wachache  kwa hiyo , watu walimpenda kwa kua alikua amejitoa kutatua tatizo hilo Kampuni ya Tesla inafanikiwa kwa kua Muanzilishi wake Ilon Musk anachukia tatizo la uchafuzi wa mazingira, kwakua magari ya kampuni yake yanatatua changamoto hio  inafanya kampuni yake kukua zaidi Chagua tatizo unalolichukia zaidi katika jamii yako, kama bidhaa au huduma yako ina tatua changamoto hiyo itakua rahisi zaidi kwako kupendwa na wateja, na hivyo kuuza zaidi huduma yako, watapokea biashara yako kama msaada Binadamu tunapenda kununua kwa mtu tunaye muamini na kumpenda kabla ya kuuza hakikisha wanakupenda wewe  kwanza

 # 2. Kuwa tofauti si bora zaidi Kuna kitu kinaitwa “Unique selling promise” Ahadi ya pekee ya kuuza maana yake ni nini? Fikilia swali hili Kwa nini ninunue kwako ? kama unauza kitu ambacho watu kumi wana nunua, kwa nini nikuchague wewe na si wengine Mmoja atajibu “ ni kwasababu bidhaa yangu ni nzuri zaidi” mwingine atasema “ ni kwasababu bidhaa yangu ina bei nafuu’ 

Tatizo la majibu hayo mawili ni kua kua na bidhaa ya bei nafuu kwenye soko hutafsiriwa kama kua na bidhaa isiyokua na kiwango  Akili ya binadamu itaona kirahisi zaidi kitu ambacho ni tofauti na si ambacho ni bora zaidi Kama wote tunauza ng’ombe ni vigumu kumshawishi mnunuzi kuwa ng’ombe wangu ni wazuri zaidi, lakini kama wana rangi ya hudhurungi tofauti itaonekana zaidi kwa mnunuzi na kumvuta macho Angalia jinsi ya kuwa tofauti na si ubora, ni vizuri kuangalia ubora lakini kama hutakua tofauti hutaweza kuwa vutia haraka wateja

 #3. Toa huduma usiuze Usijaribu kuuza toa huduma ili uweze kuuza zaidi Toa taarifa inayotakiwa, Bidhaa bora ni ile ambayo italeta  mabadiliko kwa wateja Binadamu ni wabinafsi watatoa ushirikiano kama tayari wamepata kitu toka kwako , kama umewapa huduma kwanza ni rahisi wao kununua kwako Kuwa “consultant” , kuwa mshauri na utoe huduma kwanza kwa wateja wako kabla hawajanunua toka kwako  

Chanzo: youtube channel, success secret tv


Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip