Acha kuongelea tu ndoto zako anza kuziishi
Acha kuongelea tu ndoto zako anza kuziishi
Sielewi kile ninachotaka kufanya sifanyi isipokua nisichotaka kukifanya, Hayo ni maneno ya mtume Paulo
Binadamu tuna tabia ya kufanya tusiyotaka kuyafanya na ku kushindwa kufanya tunachotakiwa kufanya
Kwa nini tunapenda kuongea tu na hatufanyi, kwa nini hakuna vitendo vya kusababisha mafanikio?, Kwa nini tunafanya kile tusichopenda na kuogopa kufanya mambo ya msingi yanayoweza kubadili maisha yetu
Nitakueleza sababu tatu kwa nini unatamani tu kufikia ndoto zako lakini hufanikiwi kuzifikia, pia ninakueleza njia za kukuwezesha kuzifikia ndoto yako
#1 Maamuzi huleta maumivu
Kuna kipindi rafiki yangu alinilipia, nilikua nimefulia sana kiasi kwamba nilimuomba pesa ya kumwandalia chakula na malazi, nilikua nikiishi nyumba ambayo haikua na umeme
Huyu rafiki aliekua akinitembelea alikua ni mtu ambaye tulikua tuna ndoto ya pamoja ya kutengeneza kampuni na kufanikiwa, pamoja na kweli kua nilikua kwenye biashara miaka nane bila mafanikio sikua na mafanikio yoyote, nlikua maskini sana miongoni mwa rafiki zangu waliokua na pesa
Nili teseka mda mrefu bila mafanikio
Tuna onta tuna tamani na tuna taka, lakini tuna epuka maamuzi kwa kua yanaleta maumivu
Maumivu huleta raha mwishoni, kwa mfano , kumbuka hadithi nliyokwambia, kuhusu mimi, niliweza kufanikiwa baada ya mwaka tu baada ya rafiki yangu kuonana nami, ndani ya mwiezi michache tu nilikua Napata pesa nyingi kuliko wao, leo natengeneza pesa zaidi
Watu wanaovaha mataji leo ni wale waliobeba misalaba ajana
Watu wanaokula raha leo walivumilia maumivu jana
Binadamu tunataka kuepuka maumivu lakini maumivu huleta furaha baadae, usiogope maumivu
#2 hatuna uhakika kama tutafanikiwa
Hauna hakika kama ndoto zako zitafanikiwa
Binadamu ni mtu ambaye ana hofu ya vitu vitakavyo tokea
Mungu yu kwapi , je anapatikana wapi,
Je nitafanikiwa kweli, hilo ni swali kila mtu hujiuliza na kushindwa kuchukua hatua
Ki ukweli hakuna uhakika kama utafanikiwa au huta fanikiwa
Watu wanaofanikiwa ni wale wanao tekeleza ndoto zao bila hofu, hata kama hawana uhakika watafanikiwa katika maisha yao
Nilipo anza ujasiriamali kila mmoja katika familia yangu alikua kinyume na mimi, watu wale walikua wana nipenda, na walijua hakuna hata mmoja katika familia yangu alie fanikiwa kufanya kile nilichotaka kufanya, hawakutaka ni feli, vipi kama ninge feli, hii ndio sababu walijalibu kunizuia ili nisiharibu maisha yangu
Lakini nilikua na ongozwa na dhamira kua umasikini ni hatari zaidi kuliko kifo
Nimekua katika sehemu ambapo umasikini ni mkubwa, najua umasikini nizaidi ya kifo
Kwahio nilipo anzisha kampuni japo sikua na uhakika, Niliamua kuwa tajiri au kufa nikijaribu kutengeneza biashara
Unapotaka kufanikiwa kwa hamu kubwa kama unataka kupumua, utafanikiwa
Kama mafanikio yako ni muhimu sana kama oksijeni utapambana mpaka mwisho
#3 Tuna tamani kungekua na njia ya kimiujiza ya kufanikiwa
Binadamu tunapenda miujiza na utajiri wa haraka, kwa kua kuna sehemu yetu ambayo haiwez jua maisha ni rahisi na yanatakiwa kuwa rahisi
Hutaweza pata kirahisi, hata kama unaamini hivo, huwezi pata kirahisi mafanikio
Maisha ni magumu, Dunia ni uwanja wa mapambano, ni sehemu ya vita. Sijui kwa nini iko ivo, lakini ndio uhalisia na siwezi kukuaminisha vinginevyo
Achana na kufikiria utajiri wa haraka, hakuna aliepata kwa urahisi, wote tuko kwenye jera moja, wote wanamatatizo na shida zao, inuka na upambane kupata unachotaka katika maisha
Acha kutegemea vitu vitakua rahisi
Pambana vita ya imani
Comments
Post a Comment