SUPU YA PWEZA SEHEMU YA O1

SUPU YA PWEZA
SEHEMU YA O1
Harson Dickson Harson
Arusha TZ
+255759148660
Mama Sabinamu, hujambo mke
wangu?
Sijambo mume wangu. Vipi kazi?
lKazi njema. Upo nyumbani?
Ndiyo mume wangu.
Eee, nenda kwenye kalenda ya
ukutani, funua nyuma kabisa, kuna
namba za simu nimeziandika,
nitumie sasa hivi.
Sawa mume wangu, alijibu mama
Sabinamu huku akikata simu.
***
Kwa hiyo ndugu zanguni, kama
nilivyokwishasema, subirini ije hiyo
namba tumpigie Ngoswe,
atakachosema ndiyo tutakuwa
tumepata majibu, baba Sabinamu
aliwaambia wageni wake.
***
Mama Sabinamu alimwamuru dereva
wa Bajaj aendeshe kwenda mbele
baada ya kumsimamisha pembeni ya
barabara ili aongee na simu na
mume wake.
Aliiseti simu vizuri, akaipiga...
Jema, umeshatoka kwenye maji?
Ndiyo mama.
Haya, nenda sebuleni, fungua
kalenda, nyuma kuna namba za simu,
nitumie sasa hivi, mama Sabinamu
alimwambia msichana wake wa
kazi.
Sawa mama.
****
Msichana wa kazi alikwenda kwenye
kalenda hiyo na kufunua nyuma
ambapo alikutana na namba kibao...
Khaa! Sasa mbona namba ni nyingi
sana? msichana wa kazi alijiuliza,
akawaza kumpigia mama Sabinamu.
Mama, mbona namba zipo nyingi?
Zipo nyingi?
Ndiyo mama.
Nitumie zote.
Haya.
****
Baba Sabinamu alipoona dakika saba
zimekatika bila kutumiwa namba
hizo alimpigia tena mkewe lakini
hakupokea, akakasirika kwani
alikuwa akiisubiri sana namba hiyo.
Mama Sabinamu baada ya kutumiwa
namba zote, na yeye alizituma kwa
mume wake akamsindikizia na
ujumbe uliosema...
Nimekuta namba nyingi, nimeona
nikutumie zote.
Baba Sabinamu alizidi kukasirika,
akampigia...
Halo mume wangu...
We mama Sabinamu una akili
kweli?
Kwa nini?
ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip