👄CHUZI LA PWEZA👄 SEHEMU YA 23

👄CHUZI LA PWEZA👄
SEHEMU YA 23
MTUNZI : Kizaro Mwakoba
WatsApp : +255765388806
ISNTARGAM: Kizaromwakoba
ILIPOISHIA
“Petrol hii hapa tumchome moto tumalize kazi jamani” Nikasikia sauti za vijana wakizungumza huku wakisogea karibu na alipokuwa amelala Mtaturu wangu. Jamani nyie kuna binadamu wana roho za kikatili, Duuh! Unaweza usiamini kabisa lakini ndivyo ilivyokuwa.
ENDELEA….23
“Jamani ngojeni kwanza, huyu mtu sio mwizi!” baadhi ya watu walisikika wakizungumza.
“Sio mwizi jamani hebu mtazameni vizuri” wengine nao wakadakia.
“Inawezekana sio mwizi” wakaongezeka zaidi na zaidi.
“Mwongo piga huyo ni mwizi tu!’ watu walijibishana baada ya kusikia sauti ya mume wangu akijaribu kujitetea.
“Jamani huyo ni mume wangu msimuue!” masikini ya Mungu nilipaza zaidi kasauti kangu ambako kiliingia vyema kwenye masikio ya baadhi ya wananchi.
“Hebu ngojeni kwanza jamani!” maneno ya watu waliokuwa wakisisitiza kusitishwa kwa zoezi lile yaliongezeka na kuwafanya wapunguze kichapo kile.
Walipommulika kwa tochi usoni masikini ya Mungu mume wangu alikuwa ni yeye kweli amejaa damu uso mzima.
“Jamani mimi ni Mtaturu naishi humu ndani” mume wangu alijieleza alipoona watu wakimfanyia uchunguzi.
“Jamani ni kweli anaishi humu ndani” Baadhi ya wapangaji wenzangu na majirani wengine nikawasikia wakizungumza kwa msisitizo huku wakisikitika.
Baadhi ya wananchi waliposikia maneno yale walianza kuchanguka mmoja mmoja kuondoka eneo la tukio kwa kuogopa kupata lawama la mtaa na uhasama wa majirani.
Kumbe nilipokuwa nimechomoka kwenye mikono ya shemeji Shabani na kukimbilia eneo la tukio, Shabani naye alinifuata nyuma. Alipofika pale alikuwa ni miongoni mwa wale wananchi waliokuwa wakisisitiza zoezi lile la kichapo lisitishwe.
“Mtaturu, imekuwaje?” Alihoji shemeji Shabani na kujifanya haelewi chochote kilichokuwa kimetokea pale.
“Hapana Shabani mimi sio mwizi” Mume wangu alizidi kujitetea.
“Huyo sio mwizi ni mbakaji” Mtu mmoja akapaza sauti.
“Hapana sio kweli, sikutaka kubaka mtu mimi” Mtaturu akajitetea.
“Sasa mbona tumesikia sauti ya mtu anapiga yowe kuwa anabakwa?” mzee mmoja wa makamo alihoji kwa msisitizo.
“Hapana, mimi niliona watu wanatembea tembea huku kwenye banda la kuku, sasa nikaona ni vyema niwafuatilie ili kuhakikisha usalama wetu, nilipofika hapa baada ya kuwakurupusha ndipo walipopiga kelele za kusema wanabakwa” Mume wangu alijaribu kujitetea ili aachiwe huru na majirani zake wale waliokuwa wamemuweka chini ya ulinzi.
Nilifanikiwa kufika pale alipokuwa amekaa mume wangu na kumkumbatia huku nikiangua kilio kwa uchungu.
Kutokana na hali aliyokuwa nayo mume wangu, alijikuta akisahau yote yaliyokuwa yametokea na kunikumbatia. Niliumia sana ndani ya moyo wangu kwasababu ukweli nilikuwa naufahamu mimi na shemeji Shabani tu.
Kilichofuata pale kilikuwa ni usamalia wema kutoka kwa wale wananchi ambao walikuwa ni wenye hasira kali dakika chache zilizokuwa zimepita. Kila mmoja ambaye alishiriki katika kumuadhibu alihisi kusutwa na nafsi yake. Pamoja na kwamba walikuwepo wengine ambao walilaumu sana kile kitendo cha kusitishwa kipigo kile cha mwizi kwa mume wangu.
Wengine walikuwa wamekwisha kufika na chupa zilizokuwa zimejaa Petroli kwa lengo la kumgeuza mishikaki mume wangu. Jamani nyie kuna binadamu ni wabaya ulimwenguni hapa!
Mimi na shemeji Shabani tukisaidiana na watu wengine tulimuinua mume wangu na kumkokota kuelekea ndani. Masikini mwanaume wangu alitembea kwa taabu sana hadi tulipomuingiza ndani na kumuweka kitandani.
“Pole sana mume wangu” Nilimwambia kwa sauti ya upole iliyokuwa imechanganyikana na wasiwasi, maana nilifahamu mwanaume yule alikuwa akinitafuta mimi na lile panga lake ambalo alimkosakosa nalo dada Sharifa kule kwenye banda la kuku.
Nilipatwa na kazi ya kuchemsha maji usiku ule kwaajili ya kumkandakanda majeraha mume wangu. Mtu mwingine ambaye alikuwa bega kwa bega na mimi katika mishemishe zile hakuwa mwingine bali ni shemeji Shabani. Kusema kweli ana moyo sana kaka wawatu.
“Pole sana kiongozi” Shabani alizungumza huku akijaribu kumfutafuta damu usoni.
“Dah kaka Raia ni hatari, walitaka kuutoa uhai wangu hivihivi” Alizungumza Mtaturu huku akijichua kichwani karibu na sikio.
“Kwani imekuwaje hasa maana mimi bado sijaelewa?” Shabani aliyachokoza tena maneno ambayo nilikuwa naomba muda wote yasije yakajirudia kwasababu mwisho wa siku nilielewa kabisa ingekula kwangu kwasababu mimi ndiye niliyekuwa chanzo cha yote, tena sio mimi peke yangu bali ni mimi na Shabani.
“Shabani we achatu, unajua…. Dah we acha tu!” Mume wangu alionekana kutaka kuzungumza kitu fulani lakini akaamua kupotezea.
“Hapana Best unajua wewe ni ndugu yangu, naomba unieleze ukweli” Shabani aling’angania kuelezwa ukweli.
Nilijaribu kumkata jicho ili kumzuia asiendelee na maswali yake lakini pamoja na kwamba aliniona nilivyokuwa nikimuonya lakini hakutaka kuonesha utayari wa kusitisha maswali yake kwa mume wangu, maswali ambayo ni wazi yalikuwa yakihatarisha ndoa yangu.
“Kwakweli sikutaka kuzungumza lakini kwakuwa wewe ni ndugu yangu na ni mwanaume mwenzangu ngoja tu nikueleze ukweli, uchambue mwenyewe chuya na mchele” alizungumza mume wangu kwa sauti ya chini.
“Sawa kaka we kuwa huru tu, mimi nakusikiliza” Shabani alijifanya kuzungumza kwa kujiamini.
Mume wangu alivuta pumzi na kuziachia kisha akamtazama Mtaturu usoni kwa sekunde kadhaa pasipo kuzungumza kitu.
“Kwa namna moja ama nyingeine kaka wewe unahusika kwenye balaa hili” alisema Mtaturu.
“Unasemaje?” Shemeji Shabani alihoji kwa kuhamaki. Hakutegemea kusikia maneno kama yele kutoka kinywani mwa Mtaturu.
“Ndio, Wewe na Mke wangu mnahusika” alisema Mtaturu kwa msisitizo.
“Mbona sikuelewi kaka Mtaturu?” Shabani alihoji kwa wasiwai huku akihisi kutetemeka kwa mbali.
“Ndio, wewe na mke wangu mnahusika kulaumiwa na ikibidi kuadhibiwa kwa hili mlilonisababishia” Alizungumza mume wangu na kutufanya mimi na Shabani kuingiwa na hofu ndani ya mioyo yetu.
Ukiweka comment NItaendelea kesho saa 12:00 Asubuhi
Pia tunatuma vipande vya mbele kwa Wattsap
Vipande 5 kwa 500/-
Vipande 15 kwa 1,000/ tuuu!😀
👉Namba ya Malipo 0765388806

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip