SUPU YA PWEZA SEHEMU YA 03

SUPU YA PWEZA
SEHEMU YA 03
Harson Dickson
+255759148660
Arusha TZ
Mama Sabinamu hakuwa na jinsi,
aliingia bafuni kuoga ili aondoke
zake.
Akina Miriam siku hiyo
walimshangaa sana mdogo wao
Masoud. Alikuwa akihangaika sana,
mara chumbani, mara jikoni, mara
nje.
We leo una nini kwani?
RUKA NAYO...
Niko sawa dada Miriam.
Mbona huku na kule, utadhani
hujatuona?
Hamna bwana dada, alisema
Masoud lakini uso wake ulionesha
wasiwasi mkubwa.
Masoud alikaa kwenye kochi
sambamba na dada zake, lakini
kabla hawajasalimiana sana, simu
yake iliita, alikuwa mama Sabinamu.
Sorry, nakuja.
Alikwenda chumbani kukutana na
mwanamke huyo...
Nikwambie kitu Masoud?
Niambie baby.
Siwezi kusubiri mpaka huo muda wa
kuondoka hao dada zako ndipo na
mimi niondoke, kama vipi
wasababishie waende kokote ili
nipite, kama haiatawezekana basi
nipite zangu mbele yao.
Masoud alihema sana. Hakuna kitu
asichopenda dada yake Miriam kama
yeye kujihusisha na uhusiano wa
mapenzi mapema, alitaka asome
kwanza.
Nyumba anayoishi Masoud ni ya
familia, baada ya kifo cha baba yake
na mama yake, familia hiyo yenye
watoto watatu tu, Miriam, Sharifa na
yeye Masoud iliamua kijana huyo
aishi hapo kwa kuwa Miriam na
Sharifa walikuwa na uwezo
walipanga nyumba Mikocheni.
Kwa kweli haitawezekana, alisema
Masoud huku akitingisha kichwa
akimaanisha kwamba hakuna namna
zozote za kuwafanya dada zake
waende sehemu ili mwanamke huyo
apite sebuleni kutoka nje na
kuondoka zake...
Basi nipite hapohapo sebuleni.
Mh! Baby, unajua dada zangu ni
wakali sana kwangu, sijui
KESHO Itakuwaje?
Kwa hiyo sweet we uko tayari
niachike kwa mume wangu kwa
sababu ya ukali wa dada zako siyo?
Sina maana hiyo.
Basi nipite.
Ilibidi Masoud akubali japo kwa
shingo upande, lakini akamwambia
watoke wote, wakifika sebuleni
atamtambulisha kuwa yeye ni nesi
alifika hapo kumchoma sindano ya
dozi ya mwisho.
Poa, mimi ilimradi niondoke, sasa
ukisema ni nesi, ni mwalimu wa
tuisheni utajua mwenyewe.
Masoud alitangulia mbele, mama
Sabinamu akawa nyuma, kufika
sebuleni, Miriam alishtuka kumwona
mwanamke huyo akitoka chumbani
na mdogo wake mdogo...
Huyu nani Masoud?
Ni nesi dada Miriam.
Wakati kijana huyo anasema ni nesi
dada Miriam, mwanamke huyo
mwenyewe alikuwa akitingisha
kichwa chini juu kuashiria kwamba
anachokisema Masoud ni kweli
kabisa...
Hivi Masoud ni nani unaweza
kumdanganya wewe, nesi huyu?
alihoji kwa ukali Sharifa huku
akimtaka mama Sabinamu
amwangalie yeye maana tangu
amefika hapo macho yake yalitua
kwa Miriam tu.
Mama Sabinamu alishtuka sana
kuonana na Sharifa, alimkumbuka...
Dada Miriam, huyu mwanamke
ndiyo yule niliyekwambia
alifumaniwa kwenye nyumba ya
jirani yangu na wazazi wa mvulana,
alikuwa akimchukua na kwenda naye
kwa rafiki yake naye shangingi kama
yeye na kushinda naye humo badala
ya kwenda shuleni.
Ha! Kweli?
Muulize mwenyewe si huyu hapo!
Mama Sabinamu uso ulimshuka
kwani ni kweli kabisa alikutwa na
mkasa huo wa aibu.
Ili kuficha aibu yake, alianza
kuondoka bila kuaga...
Yaani jimama zima unamfuata
mtoto wako kulala naye kitandani,
loo! Aibu gani hii? Miriam
alimsindikizia.
Nje ya nyumba hiyo, mama
Sabinamu aliona hata aibu
kusimama kusubiri Bajaj zinazopita,
alitembea haraka kuelekea
barabarani.
Bajaj zilichelewa kupita, akapanda
bodaboda ambapo njia nzima kila
walipopita gumzo alikuwa yeye kwa
jinsi alivyokaa kwenye bodaboda
hiyo.
Wewee, mpeleke afike huyo, vijana
wa kihuni walisema barabarani kwa
vile wowowo la mwanamke huyo
lilitokezea kwa nyuma na kumfanya
aonekane kituko flani.
Alipofika nyumbani alichukua namba
ya simu ya dereva huyo wa
bodaboda...
Unajua kwa sisi tunaopenda kwenda
safarisafari za haraka muhimu kuwa
na simu za watu kama nyinyi,
alisema mwanamke huyo huku
akijivuta kuingia ndani kwake.
Alibadili nguo haraka, akaingia
bafuni kuoga na kuendelea na
mambo mengine ya famillia.
Msichana wake wa kazi alishaanza
kuhisi jambo kwa bosi wake huyo,
hasa kwa kitendo chake cha
kumtuma kupeleka kalenda mbali
kiasi kile.
Huyu mama kuna kitu anakifanya
lakini mume wake hakijui, alisema
moyoni hausigeli huyo.
***
Dakika arobaini na tano baada ya
mama Sabinamu kurudi, mumewe
baba Sabinamu naye aliingia ndani
ya nyumba...
Ooo mume wangu, pole na kazi
jamani!
Asante mke wangu. Vipi za kushinda
hapa?
Nzuri tu, karibu sana.
Asante sana.
Mama Sabinamu aliinama na
kumfungua kamba za viatu mumewe
huku akichekacheka...
Asante sana, baba Sabinamu
alisema. Moyoni aliamini ana mke
kumbe ana changudoa.
***
Usiku, mumewe akiwa amelala
fofofo, mwanamke huyo alikuwa
ameshika simu akichati...
Kwani we suka unaishi wapi na
unaitwa nani vile mama Sabinamu
alianza kuchati na yule kijana dereva
wa bodaboda aliyempeleka",.
Tutaendelea hivi punde", Share Mara nyingi tujifunze SOTE like page"

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip