CHUZI LA PWEZA SEHEMU YA 6

CHUZI LA PWEZA
SEHEMU YA 6
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA
WatsApp : +255765388806
ISTARGAM: Kizaromwakoba
ILIPOISHIA
“Afadhali leo unifumbue dadaangu” nikazungumza kwa hamasa kubwa ya kufahamu sababu za wanaume wengi kuwa wabovu katika suala la kuhudumia ndoa zao.
ENDELEA….
“Mijitu imezama kwenye pombe utafikiri komba, unadhani atajiweza huyo? Wengine muda wote wanajichua utafikiri mafundi seremala anapiga msasa, mtu huyo atawezaje kuwa ngangari” Sharifa alizungumza kwa msisitizo.
“Mnh kumbe hizo ndizo sababu?” Nikahoji.
“Sio hizo tu, utakuta mamtu muda wote yanatoa moshi utafikiri matreni kwa kuvuta sigara, wengine wanakesha kuperuzi mapicha ya ngono, unafikiri mamtu ya hivyo yanapaswa kuonewa huruma?” alizungumza Sharifa na kunifumbua baadhi ya mambo ambayo nilikuwa siyafahamu.
“Kumbe mfumo wa maisha unaweza kuharibu kila kitu?” Nikazungumza kwa mshangao.
“Sababu zipo lukuki, hizo ni chache tu” Alisema Sharifa na kunifanya nimkumbuke tena mume wangu jinsi alivyokuwa mchovu na mvivu katika shughuli ile. Ni kweli kabisa mume wangu alikuwa akivuta sana sigara na kunywa pombe siku za nyuma. Inawezekana kabisa ikawa ni sababu kubwa.
“Dada Shery ngoja sasa nikaendelee na mambo mengine vyombo ndio nimekwisha maliza” Nilizungumza huku nikipanga panga vyombo kwenye beseni.
“Sawa mdogo wangu, ila wenye kukosa wanaume wa kazi walie tu!”
“Ah walie mwenzangu!” Nilijibu kinafki huku nikiinua beseni langu na kuelekea ndani.
Nilipofika kwenye korido nilihisi moyo wangu ukinipasuka kwa mshituko. Nilijikuta nikiinamisha macho yangu chini kumkwepa mwanaume ambaye alikuwa akija mbele yangu akitokea chumbani kwake. Mwanaume huyo alikuwa ni Shabani mume wa Sharifa. Kilikuwa nikitu cha kushangaza sana, Nilijikuta nikijawa na aibu kuliko kawaida yangu nilipokuwa nikikutana na mwanaume huyo. Sifahamu aibu ile ilikuwa imetokea wapi.
“Habari za saa hizi Mariamu?” Alinisabahi kwa sauti yake nzito ambayo siku hiyo niliiona kuwa ni tofauti na siku zote. Sauti ya siku hiyo ilikuwa na mvuto iliyoniletea msisimko uliosambaa kwenye mishipa yangu ya damu kutokea puani hadi kwenye unyayo. Kitu kingine kilichokuwa kikinifurahisha ni kuniita Mariamu jila langu la asili kabisa ambapo hata Mume wangu alikuwa hawezi kuniita hivyo.
“Salama tu shemu mabo vipi?” Nilijikuta nikitoa sauti tofauti na sauti yangu ya kawaida ambayo watu wengi walikuwa wameizoea. Nikamuona Shabani kama vile amegandishwa ghafla baada ya kusikia sauti yangu ile niliyokuwa nimeitolea puani. Baada ya hatua kama tatu hivi tulipopishana, nikageuka nyuma kumtazama. Kumbe nayeye alikuwa amegeuka kunitazama mimi. Tukajikuta macho yetu yakigongana.
“Nimesikia kama unaniita?” Nilijifanya kuhoji kumbe hakuna chochote nilichokuwa nimesikia bali ni kuzuga tu.
“Nilikuwa nakwambia umependeza” Shabani alijifanya kweli alikuwa amenisemesha kumbe naye alijitetea kwakuwa aligeuka kunitazama.
“Mnh jamani sheji mbona nipo kawaida tu” nilizungumza kwa sauti ya kudeka ambayo ilimfanya Shabani kulegeza macho utafikiri alikuwa amevuta ugolo.
“Haya bwana mtoto mzuri yetu macho tu, wacha wenye meno wafaidi” Shabani alizungumza maneno yaliyonichoma ndani ya moyo wangu kisha akageuka ili kuondoka. Lakini ghafla Sharifa aliingia na kutukuta.
“Tulia hivyo hivyo!” Sharifa alimwambia mume wake.
Mimi nilipoona dalili mbaya ya mambo kuharibika nikavuta hatua kutaka kuondoka mazingirayale.
“Nawewe unakwenda wapi? Rudisha maguu yako kama tembohapa!” Sharifa aliniambia baada ya kuniona nilikuwa nataka kuondoka kukimbia msala.
Nikasimama na kumtumbulia macho nikisubiri alichokuwa anataka kukifanya. Shabani naye alitaka kuondoka lakini Sharifa alimdaka shati na kumvuta.
“Usijifanye mjanja rudi hapa!”
“Tatizo nini?” Shabani alihoji.
“Mlikuwa mnazungumza nini?” Sharifa alihoji huku ameshika kiuno na kutetemeka kwa hasira.
Niliposikia maneno yale nilijifanya kuondoka kwa hasira huku nikiwa nimejawa na wasiwasi na woga tele. Nilihofia sana kufinyangwa na mwanamke yule ambaye mara kadhaa nilimsikia akinitahadharisha juu ya mume wake.
“We Malaya nimekwambia rudisha makongoro yako hapa!” Sharifa alinimbia kwa kiburi.
“Nakuheshimu Sharifa” nilimjibu kwa mkazo nikijifanya nimekasirika kumbe woga ulikuwa umenijaa.
“We mwanamke unakichaa?” Shabani alizungumza kwa hasira kumwambia mke wake ambaye alikuwa amemshikilia shati.
“Unajifanya mwanaume mbona…..”
“Sharap! inamaana nisisalimiane na watu kwasababu ya wivu wako?” Shabani alizungumza kwa hasira ambazo zilimfanya Sharifa kunywea kwa woga na wasiwasi. Alimuachia mume wake ambaye aliondoka na kumuacha amesimama akiwa na mshangao. Namimi nikatumia mwanya huo kutoweka mazingira yale.
*****
Nilishinda chumbani kwangu tokea asubuhi Sharifa aliponikuta nimesimama na mume wake. Nilikuwa nimejawa na wasiwasi kwa kiasi kikubwa sana. Mara kwa mara niliyakumbuka maneno ya Sharifa aliyokuwa akipenda kuyazungumza kuwa mwanamke ambaye angethubutu kutembea na mume wake chamoto angekiona. Hivyo niliamini kuwa mimi ndio nilikuwa wa kwanza kupokea hicho kibano ingawa hakunifumania nikifanya jambo lolote baya.
“Potelea mbali, kwani katukuta tunafanya nini?” nilizungumza huku nikipanga vyombo kabatini.
Sauti ya mlango wangu wa chumbani ukigongwa ilinishitua na kunifanya niache kazi yangu na kwende kufungua mlango. Sikuweza kuamini macho yangu kwani nilikutana uso kwa uso na Sharifa amesimama mlangoni kwangu akinitazama usoni.
Nakwambia ndugu msomaji kijuso kikaniparama nikawa kama vile kiazi cha kuchoma. Nikajisikia kufa kufa hivi ingawa roho ilikuwa inagoma kuacha mwili. Hata mate niliyojaribu kumeza pia hayakupita na kuhisi kukabwa kooni.
Je nini kitatokea?
Pia tunatuma vipande vya mbele kwa Wattsap
Vipande 5 kwa 500/
Vipande 10 kwa 1000/ tuuu!
Namba ya Malipo 0765388806.
Wengine tukutane kesho..

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip