MALKIA WA MAHABA ❤️ SEHEMU YA: 01

MALKIA WA MAHABA ❤️
SEHEMU YA: 01
🔞🔞 Chombezo* kali ya kifalme, iliyojaa mahaba, mapigano, visa na mikasa....
•••••••••••••
Farasi mweupe aliingia ndani ya kasri la kifalme taratibu juu yake akiwa ameketi malkia Yusta mwanamama mrembo sana akiwa na taji ya dhahabu kichwani mwake sambamba na gauni refu la rangi ya zambarau la kimalkia lenye kila aina ya urembo, akiwa na mapambo ya thamani kubwa mwilini mwake, kuanzia hereni masikioni mwake, mikufu shingoni mwake na bangili na kila aina ya kito alichovaa mwilini kilikuwa ni dhahabu tupu akiwa na msafara mkubwa wa walinzi wake waliokuwa juu ya farasi wao na silaha, takribani hamsini, kisha akashuka juu ya farasi huyo akipokelewa na askari waliojipanga mithili ya wachezao gwaride la kijeshi
"Uishi milele mtukufu malkia" Jenerali alimsalimia akiinamisha kichwa chake
"Kuna jipya gani tangu niondoke siku mbili hizi?" Malkia Yusta alimwuliza jenerali huyo aitwae Rabo
"Kuna vijana tumewakamata tunahisi ni wapelelezi wamekuja kuichunguza nchi yetu!" Jenerali Rabo alijibu malkia huyo Yusta akageuza shingo na kututazama
"Wapo wangapi?"
"Ishirini!"
"Ngoja nikawatazame!" Malkia Yusta aliuchukua upanga kutoka kwa mmoja wa walinzi wake na kuja tulipo
Wote tulikuwa tumefungiwa kwenye mti mmoja kwa minyororo tukiwa tumepiga magoti, nguo zetu za juu tumevuliwa zimebaki za chini tu, tukiwa vifua wazi
"Jason tunauwawa rafiki yangu!" Ebro aliniambia akitetemeka akiwa amejawa na wasiwasi akiwa anatetemeka baada ya kuona malkia huyo anakuja na upanga mkononi
"Usiogope Ebron tutapona hatuwezi kuuwawa!" Nilimfariji lakini moyoni namimi nikiwa na mashaka sana lakini sikutaka kuyaonyesha mashaka hayo
Ebron kijana mdogo kama mimi tumekutana tu baada ya kukamatwa na tukajikuta tunazungumza mambo mengi yeye akinisimulia kuwa anatoka nchi ya jirani iitwayo Fali nami nikadanganya natoka nchi hiyohiyo aliyoisema baada ya kujikuta tunaelewana lugha
Lakini haikuwa kweli mimi nimejikuta kwenye msitu ule wa mpakani tuliokamatwa baada tu ya kuvaa pete moja ambayo niliiokota ikiwa inang'aa kama dhahabu nikiwa na nia ya kuijaribu na kujikuta nimekuja kwenye maisha haya ya zamani sana nisiyoyaelewa
Nilizoea kuona magari ya kutumia injini na mafuta yenye matairi na barabara za lami lakini huku hakuna, usafiri uliopo ni farasi na magari ya farasi hakuna barabara za lami wala maghorofa, hakuna bunduki wala silaha za umeme silaha kuu ni mapanga mikuki na mishale
Hakuna umeme wala vifaa vya umeme, yani vitu vyote vya kisasa hakuna nilivyozoea kuviona, ni nchi ya kifalme, uvaaji wa aina yake hakuna suruali wala mashati wala tshirt wala raba wala viatu vya kutumbukiza, niliilaumu ile pete ambayo imenileta kwenye maisha haya mapya na ya kizamani sana
"Sasa hili kuwaachia huru ninawapatia mtihani wa kupambana na mtu mmoja mmojawenu akimshinda basi nitawaachia huru!" Malkia huyo alituambia akiwa ameushika upanga mkononi na mara hiyo hiyo tukamwona jamaa mkubwa wa miraba mnne aliyepanda hewani akija kichwani amenyoa upara na upanga mkubwa mkononi mwake, wote tukaanza kuogopa, na askari mmoja akaja na kutupatia kila mmoja wetu upanga tukifunguliwa kamba za chuma tulizofungiwa mikononi na miguuni
Masikini mimi! Hata kuushika upanga siwezi ndokwanza nilizoea kuuona tu kwenye movie hasa za kifalme kwenye televisheni lakini leo nayashuhudia kwa macho yangu maisha hayo ya kifalme
Alianza mmoja akaingia kupambana na lile lijamaa lirefu lililojazia, lakini akachezea kichapo mpaka akazimia kubebwa na askari kisha akaingia wapili mpaka watano wakiwa na mapanga lakini hakuna aliyeweza kulipiga jitu hilo na hatimae mimi nikawa mtu wa sita kuchaguliwa kupambana na upanga ambao sikuwahi kuutumia na wala sijui unashikwaje mpaka unapigana na mtu
Nilibaki natetemeka mbele ya jitu hilo ambalo lilinitazama kwa dharau nikihisi sasa kinachofuata ni kichapo mpaka nizimie maana hata kimaumbile mwili wangu ulikuwa ukiingia mara nne ya yule njemba
Wakati nikiwa nawaza waza na kutetemeka kwa hofu yule njemba alinirushia konde zito kwa mkono wake mmoja ambao ili kuufikia mkono wake huo basi inahitajika mikono yangu mitano
Nilijikuta nainama na kulikwepa konde hilo zito lililopita na upepo mkali ambalo kama lingenipata basi ningeungana na wale wengine watano waliozirai
"Unanikwepa Mimi kijana hahaha!" Yule njemba jitu la miraba minne lilicheka na kunitupia ngumi nzito ambayo nayo nilijikuta naikwepa bila kutarajia ikinipunyua punyua sikioni
Ebron pamoja na mateka wenzangu walianza kunishangilia walipoona naonyesha dalili ya kushinda ili wote tuachiwe huru, malkia Yusta, jenerali na askari wakiwa wanatazama kinachoendelea
Sikuelewa hata nimeyakwepaje kwepaje makonde yote mazito maana hata kupigana siwezi, yule njemba jitu la miraba minne lilikasirika nilipokwepa makonde yake mawili mazito ambayo yangetosha kunizimisha, likaanza kunifuata huku nikirudi kinyume nyume likiwa na nia ya kuninyanyua lakini nikainama na kujirusha nikitanguliza kichwa na kumpiga kichwa kwenye nyeti zake likapiga kelele na kujishika nikalikamata miguu ili niliangushe chini lakini nalo likaibeba juu juu likanitupa pembeni nikiangukia mgongo huku nalo likienda chini zima zima wenzangu wakanikimbilia wakishangilia
Askari walitaka kuwakamata lakini malkia akawazuia, walipofika wakaniinua wakinikung'uta kung'uta vumbi huku wakinipongeza kwa kuwaokoa akiwemo Ebron ambae hakuamini kama kweli nimeshinda mbele ya jitu lile la miraba minne
Askari walituchukua chini ya ulinzi mkali na kutupeleka mpaka kwenye nyumba ya wafungwa humohumo ndani ya kasri la malkia tukanyolewa vipara wote na kupewa nguo za kifungwa tofauti na ahadi ya kuachiliwa tuliyopewa mwanzoni, lakini tulipewa chakula kizuri na maji, wale watano ambao walipambana kabla yangu wakapigwa mpaka wakazirai walirudishwa wakishangaa waliposikia nimemshinda yule njemba wa miraba minne mimi nikiwa mdogo kuliko wote katika kundi letu, wote wakiwa na matumaini makubwa ya kuachiliwa na kurudi nchini mwao, lakini mimi nikiwa njiapanda hata nikiachiliwa sina pa kwenda katika ulimwengu huu wa zamani, hakuna mtu mmoja ninayemfahamu
Usiku uliingia tukiwa mahabusu tukizungumza na kufahamiana lakini hakuna niliyemwambia ukweli kuhusu nilipotokea maana wangenishangaa hakuna ambae angeniamini
Ghafla askari wawili wakaingia wote tukakaa sawa
"Jason tufuate haraka!" Mmoja aliniamrisha nikainuka na kuwaacha wenzangu wakiwa kimya hakuna aliyejua ninapopelekwa na hata mimi niliingiwa wasiwasi
Niliwafuata wale askari nyumanyuma wakaniingiza mpaka ndani ya kasri la malkia Yusta, wanawake wawili warembo walinishika mkono wa na wa kushoto wakaniingiza kwenye bafu moja zuri na kunivua nguo zangu nikaingizwa kwenye beseni kubwa la kuogea lililopambwa kwa rangi za kupendeza wakaanza kuniogesha
Walipomaliza walinivalisha tu kitambaa mithili ya taulo kuanzia kiunoni kwenda chini, juu nikibaki kifua wazi wakaipaka mafuta ya kunukia na marashi kisha wakanitoa bafuni wakiwa wamenishika mkono mpaka kwenye sebule kubwa ya kasri la malkia ambapo walinikabidhi kwa mwanamke mwingine aliyenipeleka mpaka kwenye mlango mkubwa wa chumba kimoja
"Mtukufu malkia!" Aliita mlangoni
"Mwache aingie!" Sauti ilimjibu mwanamke huyo akanifungulia mlango nikaingia kwenye chumba hicho kikubwa cha malkia
Lakini nilishangaa nilipomshuhudia mwanamama huyo malkia akiwa uchi, hana nguo hata moja akiwa amesimama mbele yangu karibu na kitanda chake kikubwa, amenipa mgongo......
Vipi stori mwanzo umeeleweka???!!!
Fanya kudondosha #Comment na #Like yako!

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU VISABABISHI VYA UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)

Fahamu faida 30 za mmea wa Aloe Vera

Catnip