SUPU YA PWEZA SEHEMU YA O1 Harson Dickson Harson Arusha TZ +255759148660 Mama Sabinamu, hujambo mke wangu? Sijambo mume wangu. Vipi kazi? lKazi njema. Upo nyumbani? Ndiyo mume wangu. Eee, nenda kwenye kalenda ya ukutani, funua nyuma kabisa, kuna namba za simu nimeziandika, nitumie sasa hivi. Sawa mume wangu, alijibu mama Sabinamu huku akikata simu. *** Kwa hiyo ndugu zanguni, kama nilivyokwishase ma, subirini ije hiyo namba tumpigie Ngoswe, atakachosema ndiyo tutakuwa tumepata majibu, baba Sabinamu aliwaambia wageni wake. *** Mama Sabinamu alimwamuru dereva wa Bajaj aendeshe kwenda mbele baada ya kumsimamisha pembeni ya barabara ili aongee na simu na mume wake. Aliiseti simu vizuri, akaipiga... Jema, umeshatoka kwenye maji? Ndiyo mama. Haya, nenda sebuleni, fungua kalenda, nyuma kuna namba za simu, nitumie sasa hivi, mama Sabinamu alimwambia msichana wake wa kazi. Sawa mama. **** Msichana wa kazi alikwenda kwenye kalenda hiyo na kufunua nyuma ambapo alikutana na namba kibao... Khaa!...