OKSIJENI NI BLOG. INAYOKUPATIA MAARIFA KATIKA NYANJA NYINGI KAMA VILE SAYANSI, ELIMU,TIBA,UJASILIAMALI NA KOMPYUTA. KWETU MAARIFA NI UHAI . ILI KUPATA HUDUMA NA MSAADA WA KITEKNOLOJIA. TUPIGIE SIMU AU TUTAFUTE WHATSSAP KWA NAMBA 0629811027
NAMNA AMBAVYO MTU ANAPATA UGONJWA WA NGIRI (HERNIA) TATIZO LA NGIRI (HERNIA) Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo. Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni). Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na
Tarakilishi/ kompyuta Ni mashine ya kielektroniki yenye uwezo wa kipokea kichakata, kuhifadhi na kutoa taarifa kwa haraka kulingana na maelekezo -Huwekwa programu -Hutumika kurahisisha kazi mbalimbali Kazi za msingi za tarakilishi Kuingiza au kupokea data au taarifa Kutenda na kuchakata data au taarifa Kuhudadhi data au taarifa Kutoa au kuonesha matokeo ya kazi au taarifa Aina za tarakilishi Kuna aina mbili za tarakilishi: tarakilishi ya mezani na tarakilishi mpakato Tarakilishi ya mezani -Vifaaa vyake vimetenganishwa -vifaa vyake ni kashamfumo, kibodi , kiteuzi na monita Tarakilishi mpakato -Vifaa vyake vyote vimeunganishwa -Hurahisiha ubebaji na matumizi mahali popote Kazi za vifaa vya tarakilishi Kashamfumo : Huifadhi na kulinda vifaa vyote vya kielektroniki Kichakato kikuu : hupokea na kuchakata kazi zote zinazoingia kwenye tarakilishi Kiteuzi au mausi: Hutumia kielekezi kumwelekeza mtumiaji wa tarakilishi kuelekeza tendo fulani analotaka kufanya Kibodi : Hutumika kuingiza dat
Comments
Post a Comment